| Table of Contents | Words: Alphabetical - Frequency - Inverse - Length - Statistics | Help | IntraText Library |
Umoja wa Mataifa ofisi ya idara ya habari Taarifa ya Ulimwengu juu ya Haki za Binadamu IntraText CT - Text |
|
|
|
Umoja wa Mataifa ofisi ya idara ya habari Taarifa ya Ulimwengu juu ya Haki za BinadamuKatika Disemba 10, 1948, Baraza kuu la Umoja wa Mataifa lilikubali na kutangaza Taarifa ya Ulimwengu juu ya Haki za Binadamu. Maelezo kamili ya Taarifa hiyo yamepigwa chapa katika kurasa zifuatazo. Baada ya kutangaza taarifa hii ya maana Baraza Kuu lilizisihi nchi zote zilizo Wanachama wa Umoja wa Mataifa zitangaze na "zifanye ienezwe ionyeshwe, isomwe na ielezwe mashuleni na katika vyuo vinginevyo bila kujali siasa ya nchi yo yote." UtanguliziKwa kuwa kukiri heshima ya asili na haki sawa na binadamu wote ndio msingi wa uhuru, haki na amani duniani, Kwa kuwa kutojali na kudharau haki za binadamu kumeletea vitendo vya kishenzi ambavyo vimeharibu dhamiri ya binadamu na kwa sababu taarifa ya ulimwengu ambayo itawafanya binadamu wafurahie uhuru wao wa kusema, kusadiki na wa kutoogopa cho chote imekwisha kutangazwa kwamba ndio hamu kuu ya watu wote, Kwa kuwa ni lazima, ili mtu asishurutizwe kuomba msaada kutokana na maasi ya kupinga dhuluma na uonevu, kwamba haki za binadamu ziwe chini ya ulinzi wa sheria, Kwa kuwa ni lazima kabisa kuendeleza uhusiano wa kirafiki kati ya mataifa, Kwa kuwa watu wa Umoja wa Mataifa wamethibitisha tena katika Mkataba wao imani yao katika haki za asili, heshima na thamani ya binadamu na katika usawa wa haki kwa wanaume na wanawake, na kwa sababu wamekata shauri la kuendeleza mambo ya starehe na hali bora za maisha ya watu kwa kuwa na uhuru zaidi, Kwa kuwa Nchi zilizo Wanachama zimeahidi, kwa kushirikiana na Umoja wa Mataifa, kukuza na kuheshimu haki za binadamu na uhuru wake wa asili, Kwa kuwa kuzitambua haki hizi na uhuru huu ni jambo la maana sana kua kutimiza ahadi hiyo, Kwa hiyo basi,
|
Table of Contents | Words: Alphabetical - Frequency - Inverse - Length - Statistics | Help | IntraText Library |
Best viewed with any browser at 800x600 or 768x1024 on Tablet PC IntraText® (V89) - Some rights reserved by EuloTech SRL - 1996-2007. Content in this page is licensed under a Creative Commons License |