101 - 109
101. Sema: Angalieni yaliomo mbinguni na kwenye ardhi! Na
Ishara zote na maonyo hayawafai kitu watu wasio amini.
102. Basi, je! Wanangojea jingine ila kama yaliyo tokea
siku za watu walio pita kabla yao? Ngojeni! Nami ni pamoja nanyi katika wanao
ngoja.
103. Kisha Sisi huwaokoa Mitume wetu na walio amini. Ndio
kama hivyo, inatustahiki kuwaokoa Waumini.
104. Sema: Enyi watu! Ikiwa nyinyi mnayo shaka katika Dini
yangu, basi mimi siwaabudu mnao waabudu nyinyi badala ya Mwenyezi Mungu. Lakini
mimi namuabudu Mwenyezi Mungu anaye kufisheni. Na nimeamrishwa niwe miongoni
mwa Waumini.
105. Na uelekeze uso wako kwenye Dini ya Kweli, wala usiwe
katika washirikina.
106. Na wala usiwaombe wasio kuwa Mwenyezi Mungu ambao
hawakufai kitu wala hawakudhuru. Ukifanya hivyo basi utakuwa miongoni mwa walio
dhulumu.
107. Na Mwenyezi Mungu akikugusisha madhara, basi hapana wa
kukuondolea ila Yeye. Na akikutakia kheri, basi hapana awezaye kurudisha
fadhila yake. Huifikisha kwa amtakaye katika waja wake, na Yeye ni Mwenye
kusamehe, Mwenye kurehemu.
108. Sema: Enyi watu! Haki imekwisha kukujieni kutoka kwa
Mola wenu Mlezi. Basi anaye ongoka anaongoka kwa faida ya nafsi yake, na anaye
potea anapotea kwa khasara ya nafsi yake. Na mimi si mwakilishi juu yenu.
109. Na wewe fuata yanayo funuliwa kwako kwa wahyi. Na
vumilia mpaka Mwenyezi Mungu ahukumu, na Yeye ndiye mbora wa mahakimu.
|