11. SURAT HUD
(Imeteremka
Makka)
Surat
Hud ni Sura ya Makka. Ina Aya 123. Imeanza kwa kuisifu , na kumuabudu Mwenyezi
Mungu peke yake, na kuonya, na kubashiria. Kisha ikabainisha uwezo wa Mwenyezi
Mungu na kuwa Yeye ndiye Mola Mlezi. Na ikaeleza hali za watu katika kuzipokea
kwao neema zake Mola Mlezi, na adhabu zake. Kisha ikataja cheo cha Qur'ani, na
kufuru za makafiri bila ya udhuru wowote kwa ukafiri wao, na malipo ya Waumini.
Naye Subhanahu baada ya hayo amesimulia hadithi za Manabii, na majadiliano ya
kaumu zao nao, na kuwateremkia makafiri adhabu ya duniani na kuokoka kwa
Waumini. Subhanahu wa Taa'la akataja hadithi ya Nuhu kwa kupambanua zaidi
kuliko ilivyo kuwa katika Surat Yunus. Humu imeelezwa fikra za kafiri na inadi
yake, na imebainishwa ilivyo mteremkia chuki. Na baada ya hadithi ya Nuhu
Mwenyezi Mungu Subhanahu ametaja kisa cha A'ad pamoja na Nabii wa Mwenyezi
Mungu Hud, kwa kueleza wazi mawazo ya ukafiri, na yaliyo wateremkia makafiri
juu ya kuwa walikuwa na nguvu na wakali.
Kisha kikatajwa mfano wa hayo kisa cha Nabii wa Mwenyezi Mungu, Saleh pamoja na
kabila la Thamud, na tena kisa cha Nabiyyu Llah na rafiki yake, Ibrahim. Kisha
hadithi wa Nabiyyu Llah, Lut'. Kisha kisa cha Nabiyyu Llah, Shua'ib.
Kisha Subhanahu wa Taala ametaja nini mafunzo ya hadithi hizi za kweli, na
akamalizia Subhanahu kwa kuwataka Waumini watende mema, na wangojee malipo.
Tena ukatajwa ujuzi ulio kamilika wa Mwenyezi Mungu Aliye takasika na kutukuka,
na waajibu wa kumtegemea Yeye.
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU
MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU
|