19. SURAT MARYAM
(Imeteremka
Makka)
Hii ni Sura iliyo teremka Makka, na hamna Aya
za Madina ila Aya 57 na 71. Hisabu
ya Aya zake ni 98. Imeanzia kwa harufi moja moja kama Sura nyingi nyenginezo.
Ndani ya Sura hii kipo kisa cha kuzaliwa Yahya bin Zakariya (Alayhima Ssalam).
Zakariya alitamani mwana na hali kesha fikilia ukongwe na mkewe ni tasa. Na
kimetajwa pia kisa cha Bibi Bikra Maryam (A.S.) na kumzaa kwake Masihi (A.S.).
Kisha kikatajwa kisa cha Ibrahim (A.S) na Wito wake kulingania Upweke wa
Mwenyezi Mungu, na alivyo mtaka babaake aache kuabudu masanamu, na majibizano
yao yaliyo jiri kwa ajili ya masanamu, na madaraka ya Shet'ani.
Pia wameashiriwa Manabii wengine katika dhuriya za Ibrahim, nao Ismail na
Is-haq na dhuriya wa Is-haq. Tena kikagusiwa kisa cha Idris (A.S.). Na tena
Mwenyezi Mungu Subhanahu akataja khabari za walio fuatia wakaja baada ya
Manabii, watu wat'iifu na wengine maasi. Na akataja kuwa Pepo ndiyo malipo ya
Waumini, na Moto ni malipo ya makafiri, na akazitaja hali za makafiri katika
Jahannamu. Na tena Subhanahu akagusia ya wapotovu wanao sema kwamba Mwenyezi
Mungu ana mwana.
Na Subhanahu amebainisha cheo cha Qur'ani, na amewaonya makafiri, na amepiga
mifano ya watavyo teketea wanao waasi Manabii. Na akaashiria kwamba hao
wamepotea kabisa, hawakuacha hata ukumbusho.
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU
MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU
|