101 - 112
101. Ama wale ambao wema wetu umewatangulia, hao
watatenganishwa na hayo.
102. Hawatausikia mvumo wake, na wao watadumu katika yale
zinayo yatamani nafsi zao.
103. Hicho
Kitisho Kikubwa hakito wahuzunisha. Na Malaika watawapokea (kwa kuwaambia): Hii
ndiyo Siku yenu mliyo kuwa mkiahidiwa!
104. Siku
tutakapo zikunja mbingu kama mkunjo wa karatasi za vitabu. Kama tulivyo
anza umbo la mwanzo tutalirudisha tena. Ni ahadi iliyo juu yetu. Hakika Sisi ni
watendao.
105. Na hakika tulikwisha andika katika Zaburi baada ya Kumbukumbu,
ya kwamba nchi watairithi waja wangu walio wema.
106. Hakika katika haya yapo mawaidha kwa watu wafanyao
ibada.
107. Nasi hatukukutuma ila uwe ni Rehema kwa walimwengu
wote.
108. Sema: Hakika imefunuliwa kwangu ya kwamba hakika Mungu
wenu ni Mungu Mmoja tu. Je!
Mmesilimu?
109. Na kama
wakigeuka, basi sema: Nimekutangazieni sawa sawa, wala sijui yako karibu au
mbali hayo mliyo ahidiwa.
110. Hakika Yeye
anajua kauli ya dhaahiri na anajua myafichayo.
111. Wala sijui
pengine huu ni mtihani tu kwenu na starehe mpaka muda kidogo.
112. Sema: Mola wangu Mlezi! Hukumu kwa haki. Na Mola wetu Mlezi ni Mwingi wa
Rehema, aombwaye msaada juu ya mnayo yazua.
|