22. SURATUL HAJJ
(Imeteremka
Madina)
Sura hii ni ya Madina ila Aya 52, 53, 54, na 55. Aya zake ni sabiini na
nane. Imeanzia kwa kuwaonya watu wamkhofu Mwenyezi Mungu, na kukumbusha vitisho
vya Kiyama, na kuwajuilisha wanao bisha kwa upotovu na ujinga, na hayo
yakafuatia kuletwa dalili za kufufuliwa, kwa kuleta sura ya mabadiliko katika
kuumbwa binaadamu na kukua kwa mimea, na ikaeleza upinzani kumpinga Mwenyezi
Mungu, na matokeo yake. Na ikataja khabari ya Hija na kutukuza ibada zake. Na
baada ya hayo Mwenyezi Mungu akaruhusu kupigana vita vya kujitetea. Na
akafuatilizia hayo kumpoza Mtume s.a.w. kwa masaibu yaliyo kuwa yanampata kwa
watu wake, kwa kutaja dhiki na mateso yaliyo wapata Mitume wa kabla yake. Na
Aya za Sura hii zikabainisha dalili za uweza wake Mwenyezi Mungu Mtukufu na
upweke wake, na mipaka ya kazi ya Mitume. Na kwamba hili ni onyo lisilo
kimbilika. Na katika mwisho wa Sura wakasema hao wanao ambiwa ni washirika wa
Mwenyezi Mungu kwa kuzizuga akili za washirikina, kwamba hawawezi hata kuumba
kiumbe kinyonge kabisa, naye ni nzi. Na nzi akiwapokonya kitu hawawezi kukipata
kwake. Na Sura ikahimiza Sala, na Zaka, na Ibada, na Jihadi, bila ya kukusudia
maovu. Kwani hii ni Dini ya baba yenu Ibrahim aliye mzaa Ismail, ambaye
kutokana naye ndio wakazalika ukoo wa A'dnan. Na matokeo ya mambo yenu ni kuwa
Mtume wenu akushuhudieni kwa kukufikishieni Ujumbe, na nyinyi mtoe ushahidi juu
ya watu walio kwisha tangulia kwamba Mitume wao waliwafikishia Ujumbe kama
ilivyo kujieni katika Qur'ani. Na Sura ikakhitimisha kwa kutaka kushikamana na
Mwenyezi Mungu. Kwani Yeye ndiye bora ya Mlinzi, na bora ya Mwenye kunusuru.
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU
|