23. SURATUL MUUMINUN
(Imeteremka
Makka)
HII NI SURA iliyo teremka Makka. Aya zake ni mia na kumi na nane. Imeanza
kwa kuthibitisha mafanikio ya Waumini, na ikafuatia kueleza sifa zao. Kisha
ikataja asli ya kuumbwa mwanaadamu, na kubadilika kwake kwa kukua, na
kuzalikana vizazi vyake, na baadhi ya mambo yanayo dhihirisha uwezo wa Mwenyezi
Mungu Mtukufu. Tena zikafuatia hadithi za Manabii zinazo fanana kwa umoja wa
ujumbe na umoja wa binaadamu, ijapo kuwa watu wanga khitalifiana baina ya wanao
kubali na wanao kengeuka. Na sura hii imeeleza khabari za mwenye kutaka
uwongofu, na mwenye kupotoka, na msimamo wa washirikina mbele ya Nabii s.a.w.
Tena ikaingia kueleza yanayo onekana ya uwezo wa Mwenyezi Mungu katika hukumu
za kumuumba mwanaadamu. Na Mwenyezi Mungu Subhanahu kaingia kuwauliza watu
wamjibu kwa kutumia akili zao za maumbile kwa yanayo thibitisha kuwepo kwake,
na kuthibitisha Ungu wake. Kisha Sura hii ikaeleza hali za watu itavyo kuwa
Siku ya Kiyama, na kwamba wao watahisabiwa, na watafanyiwa uadilifu. Tena Sura
inakhitimisha kubainisha Utukufu wake Subhanahu wa Taa'la, na kumnabihisha
Nabii wake aombe maghfira na rehema kutokana na Mbora wa wenye kurehemu.
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU
|