101 - 118
101. Basi litapo pulizwa baragumu hapo hautakuwapo ujamaa
baina yao siku hiyo, wala hawataulizana.
102. Ama wale ambao mizani zao zitakuwa nzito, hao ndio
wenye kufanikiwa.
103. Na wale ambao mizani zao zitakuwa nyepesi, hao ndio
walio zitia khasarani nafsi zao, na katika Jahannamu watadumu.
104. Moto utababua nyuso zao, nao watakuwa na nyuso zilizo
kunjana.
105. Je! Hazikuwa Aya zangu mkisomewa, na nyinyi
mkizikanusha?
106. Mola wetu Mlezi! Tulizidiwa na uovu wetu na tukawa
watu tulio potea.
107. Mola wetu Mlezi! Tutoe humu Motoni. Na tufanyapo tena basi
kweli sisi ni wenye kudhulumu.
108. Atasema Mwenyezi Mungu: Tokomeeni humo, wala
msinisemeze.
109. Bila ya shaka lilikuwapo kundi katika waja wangu
likisema: Mola wetu Mlezi! Tumeamini; basi tusamehe na uturehemu, nawe ndiwe
Mbora wa wanao rehemu.
110. Lakini nyinyi mliwakejeli hata wakakusahaulisheni
kunikumbuka, na mlikuwa mkiwacheka.
111. Hakika Mimi leo nimewalipa kwa vile walivyo subiri.
Bila ya shaka hao ndio wenye kufuzu.
112. Atasema: Mlikaa muda gani katika ardhi kwa hisabu ya
miaka?
113. Watasema: Tulikaa siku moja au sehemu ya siku. Basi waulize wanao weka hisabu.
114.
Atasema: Nyinyi hamkukaa huko duniani ila kidogo, laiti ingeli kuwa mnajua.
115. Je!
Mlidhani ya kwamba tulikuumbeni bure na ya kwamba nyinyi kwetu hamtarudishwa?
116.
Ametukuka Mwenyezi Mungu, Mfalme wa Haki, hapana mungu ila Yeye, Mola Mlezi wa
A'rshi Tukufu.
117. Na
anaye muomba - pamoja na Mwenyezi Mungu - mungu mwenginewe hana ushahidi wa
hili; basi bila ya shaka hisabu yake iko kwa Mola wake Mlezi. Kwa hakika
makafiri hawafanikiwi.
118. Nawe sema: Mola wangu Mlezi! Samehe na urehemu nawe ni
Mbora wa wanao rehemu.
|