201 - 227
201. Hawataiamini mpaka waione adhabu chungu.
202. Basi itawafikia kwa ghafla, na hali hawana khabari.
203. Na watasema: Je, tutapewa muhula?
204. Basi, je, wanaihimiza adhabu yetu?
205. Waonaje kama tukiwastarehesha kwa miaka,
206. Kisha yakawafikia waliyo kuwa wakiahidiwa,
207. Yatawafaa nini yale waliyo stareheshewa?
208. Wala hatukuangamiza mji wo wote ila ulikuwa na
waonyaji -
209. Kuwa ni ukumbusho. Wala Sisi hatukuwa wenye kudhulumu.
210. Wala Mashet'ani hawakuteremka nayo,
211. Wala haitakiwi kwao, na wala hawawezi.
212. Hakika hao wametengwa na kusikia.
213. Basi usimwombe mungu mwingine pamoja na Mwenyezi Mungu
ukawa miongoni mwa watakao adhibiwa.
214. Na uwaonye jamaa zako walio karibu nawe.
215. Na watwae kwa upole wanao kufuata miongoni mwa
Waumini.
216. Na ikiwa watakuasi basi sema: Mimi najitenga mbali na
hayo mnayo yatenda.
217. Na umtegemee Mtukufu Mwenye nguvu Mwenye kurehemu.
218. Ambaye anakuona unapo simama,
219. Na mageuko yako kati ya wanao sujudu.
220. Hakika Yeye ndiye Mwenye kusikia Mwenye kujua.
221. Je! Nikwambieni nani wanawashukia Mashet'ani?
222. Wanamshukia kila mzushi mkubwa mwingi wa dhambi.
223. Wanawapelekea yale wanayo yasikia; na wengi wao ni
waongo.
224. Na watungaji mashairi ni wapotofu ndio wanawafuata.
225. Je! Huwaoni kwamba wao wanatangatanga katika kila
bonde?
226. Na kwamba wao husema wasiyo yatenda?
227. Isipo kuwa wale walio amini, na wakatenda mema, na
wakamkumbuka Mwenyezi Mungu kwa wingi, na wakajitetea wanapo dhulumiwa. Na
wanao dhulumu watakuja jua mgeuko gani watakao geuka.
|