Table of Contents | Words: Alphabetical - Frequency - Inverse - Length - Statistics | Help | IntraText Library

Qu'rani

IntraText CT - Text

  • 27. SURAT AN-NAML
Previous - Next

Click here to hide the links to concordance

27. SURAT AN-NAML

(Imeteremka Makka)

SURA AN-NAML ni ya Makka. Aya zake ni 93.
Imeanza kwa harufi za kutamkwa, kukumbusha cheo cha Qur'ani ambayo imetoka katika jinsi ya maneno ya Kiarabu. Na juu ya hivyo imewashinda hao Waarabu kuleta mfano wake. Na tena pia ni kama kumzindua aliye ghafilika aisikilize. Baada yake kimekuja kisa cha Musa a.s. Na imetajwa baadhi ya miujiza yake, na kisa cha Daudi a.s. na kurithiwa kwake na mwanawe, Mfalme Sulaiman, na kukusanyika majini, na watu, na ndege kwa ajili yake. Na imetajwa kufahamu kwake Sulaiman maneno ya wanyama, na shukrani yake kwa neema hii. Kisha kutoweka ndege Hud-hud, na akaja na kisa cha Balqis, na kuabudu kwake bibi huyu na watu wake kuliabudu jua. Tena Sulaiman akampelekea barua, naye akamjibu kwa kumpelekea zawadi baada ya kushauriana na watu wake, na ikaelezwa kuletwa kiti chake cha enzi kwa njia ya mwenye ilimu ya Kitabu, na kuingia kwake huyo bibi katika qasri (jumba la kifalme) la Sulaiman, nalo likamshitua, na akatangaza ut'iifu wake na Imani yake kumuamini Sulaiman.
Na Sura hii imetaja hadithi ya Saleh a.s. na kaumu yake, na hadithi ya Lut'i a.s. na kaumu yake, na kuvuka kwake, na kuangamia kwa mafisadi. Na Sura tukufu hii imezindua ziangaliwe dalili za aliye umba mbingu na ardhi zenye kuthibitisha uwezo wake na upweke wake.
Na ikaashiria cheo cha katika kazi ya Daa'wa (Wito), na vipi washirikina wanavyo ipuuza juu ya kuwa muujiza wake umekamilika. Na imetaja yatakayo kuwa atapo toka mnyama akisema na watu kuwa walikuwa hawana yakini ya Ishara zetu. Kisha Sura ikaelekea ulimwengu, na vipi watavyo fazaika waliomo wakati wa mpulizo wa kufufuliwa na kukusanywa. Na ikanabihisha hali ya ardhi, na kwamba milima yake inakwenda kama yaendavyo mawingu, na ikasimulia yanayo mfuatia Mtume katika kazi yake ya Daa'wa, na kwamba ni waajibu Mwenyezi Mungu Aliye takasika asifiwe.

KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU




Previous - Next

Table of Contents | Words: Alphabetical - Frequency - Inverse - Length - Statistics | Help | IntraText Library

Best viewed with any browser at 800x600 or 768x1024 on Tablet PC
IntraText® (V89) - Some rights reserved by EuloTech SRL - 1996-2007. Content in this page is licensed under a Creative Commons License