Table of Contents | Words: Alphabetical - Frequency - Inverse - Length - Statistics | Help | IntraText Library

Qu'rani

IntraText CT - Text

  • 28. SURAT AL-QAS'AS'
Previous - Next

Click here to hide the links to concordance

28. SURAT AL-QAS'AS'

(Imeteremka Makka)

SURA YA AL-QAS'AS' ni ya 28 katika mpango wa Msahafu. Nayo ni Sura ya Makka. Aya zake ni thamanini na nane.
Imetaja kwa kufafanua yaliyo kwisha tajwa kabla yake kwa jumla katika mambo ya Musa a.s. tangu kuzaliwa kwake katika enzi ya Firauni. Na Firauni alikuwa akiwauwa watoto wanaume wa Bani Israili kwa kukhofu asije tokea Nabii miongoni mwao atakaye teketeza ufalme wake.
Kisha yakaelezwa yaliyo tokea kukhusu kulelewa kwake Musa katika nyumba ya Firauni, mpaka alipo itoka Misri kukimbiza roho yake kwenda Madiani katika nchi ya Shamu. Na tena akarejea na mkewe, binti wa Shuaibu a.s.
Kisha yakatajwa ya mazungumzo ya Mwenyezi Mungu na Musa, na kumteuwa yeye kwa kumpa Utume, na mambo yaliyo tokea yaliyo mkhusu Firauni na wachawi wake pamoja na Musa, mpaka Mwenyezi Mungu alipo mzamisha Firauni na jeshi lake. Na Musa na Wana wa Israili walio kuwa pamoja naye wakaokoka. Kisha yaliyo watokea Wana wa Israili pamoja na Musa na nduguye Harun. Na zimetajwa pia khabari za walio kadhibisha kama Qaaruni na makafiri wengine walio watangulia. Na kwa maelezo haya yaliyo kusanya khabari mbali mbali ndio Sura hii ikaitwa Surat al-Qas'as', yaani Sura ya Visa, au Hadithi.

KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU




Previous - Next

Table of Contents | Words: Alphabetical - Frequency - Inverse - Length - Statistics | Help | IntraText Library

Best viewed with any browser at 800x600 or 768x1024 on Tablet PC
IntraText® (V89) - Some rights reserved by EuloTech SRL - 1996-2007. Content in this page is licensed under a Creative Commons License