51 - 83
51. Na litapulizwa barugumu, mara watatoka makaburini
wakikimbilia kwa Mola wao Mlezi.
52. Watasema: Ole wetu! Nani aliye tufufua kwenye malazi
yetu? Haya ndiyo aliyo yaahidi Mwingi wa Rehema na wakasema kweli Mitume.
53. Haitakuwa ila ukelele mmoja tu, mara wote
watahudhuruishwa mbele yetu.
54. Basi leo nafsi yoyote haitadhulumiwa kitu, wala
hamtalipwa ila yale mliyo kuwa mkiyatenda.
55. Hakika watu wa Peponi leo wamo shughulini, wamefurahi.
56. Wao na wake zao wamo katika vivuli wameegemea juu ya
viti vya fakhari.
57. Watapata humo kila namna ya matunda na watapata kila
watakacho kitaka.
58. "Salama!" Hiyo ndiyo kauli itokayo kwa Mola
Mlezi Mwenye kurehemu.
59. Na enyi wakosefu! Jitengeni leo!
60. Je! Sikuagana nanyi, enyi wanaadamu, kuwa msimuabudu
Shet'ani? Hakika yeye ni adui dhaahiri kwenu.
61. Na ya kwamba mniabudu Mimi? Hii ndiyo Njia Iliyo
Nyooka.
62. Na bila ya shaka yeye amekwisha lipoteza kundi kubwa
miongoni mwenu. Je, hamkuwa
mkifikiri?
63. Hii basi
ndiyo Jahannamu mliyo kuwa mkiahidiwa.
64. Ingieni leo
kwa vile mlivyo kuwa mkikufuru.
65. Leo tunaviziba
vinywa vyao, na iseme nasi mikono yao, na itoe ushahidi miguu yao kwa waliyo
kuwa wakiyachuma.
66. Na tungeli
penda tungeli yafutilia mbali macho yao, wakawa wanaiwania njia. Lakini wange
ionaje?
67. Na tungeli
taka tunge wageuza sura hapo hapo walipo, basi wasinge weza kwenda wala kurudi.
68. Na tunaye
mzeesha tunamrudisha nyuma katika umbo. Basi je! hawazingatii?
69. Wala
hatukumfundisha (Muhammad) mashairi, wala hayatakikani kwake hayo. Haukuwa huu
ila ni ukumbusho na Qur'ani inayo bainisha.
70. Ili imwonye
aliye hai, na neno litimie juu ya makafiri.
71. Je! Hawaoni
kwamba tumewaumbia kutokana na iliyo fanya mikono yetu wanyama wa mifugo, na
wao wakawa wenye kuwamiliki.
72. Na Sisi tukawadhalilishia. Basi baadhi yao wako wanao
wapanda, na baadhi yao wanawala.
73. Na wao wanapata kwao manufaa na vinywaji. Basi je,
hawashukuru?
74. Na wameishika miungu mingine badala ya Mwenyezi Mungu
ili ati wapate kusaidiwa!
75.
Hawataweza kuwasaidia. Bali hao ndio watakuwa askari wao watakao hudhurishwa.
76. Basi
maneno yao yasikuhuzunishe. Hakika Sisi tunayajua wanayo yaweka siri na wanayo
yatangaza.
77. Kwani
mwanaadamu haoni ya kwamba Sisi tumemuumba yeye kutokana na tone la manii?
Kisha sasa yeye ndio amekuwa ndiye mgomvi wa dhaahiri!
78. Na
akatupigia mfano, na akasahau kuumbwa kwake, akasema: Ni nani huyo atakaye
ihuisha mifupa nayo imekwisha mung'unyika?
79. Sema:
Ataihuisha huyo huyo aliye iumba hapo mara ya mwanzo. Na Yeye ni Mjuzi wa kila
kuumba.
80. Aliye
kujaalieni kupata moto kutokana na mti wa kijani nanyi mkawa kwa huo mnawasha.
81. Kwani
aliye ziumba mbingu na ardhi hawezi kuwaumba mfano wao? Kwani! Naye ndiye
Muumbaji Mkuu, Mjuzi.
82. Hakika
amri yake anapo taka kitu ni kukiambia tu: Kuwa! Na kikawa.
83. Basi
Ametakasika yule ambaye mkononi mwake umo Ufalme wa kila kitu; na kwake Yeye
mtarejeshwa.
|