1 - 50
1. Naapa kwa wanao jipanga kwa safu.
2. Na kwa wenye kukataza mabaya.
3. Na kwa wenye kusoma Ukumbusho.
4. Hakika Mungu wenu bila ya shaka ni Mmoja.
5. Mola Mlezi wa mbingu na ardhi, na yaliyomo kati yao, na
ni Mola Mlezi wa mashariki zote.
6. Hakika Sisi tumeipamba mbingu ya karibu kwa pambo la
nyota.
7. Na kulinda na kila shet'ani a'si.
8. Wasiweze kuwasikiliza viumbe watukufu. Na wanafukuzwa
huko kila upande.
9. Wakifurushwa. Na wanayo adhabu ya kudumu.
10. Isipo kuwa anaye nyakua kitu kidogo, na mara humfwatia
kimondo kinacho ng'ara.
11. Hebu
waulize: Je! Wao ni wenye umbo gumu zaidi au hao wengine tulio waumba. Hakika
Sisi tuliwaumba wao kwa udongo unao nata.
12. Bali
unastaajabu, na wao wanafanya maskhara.
13. Na wanapo
kumbushwa hawakumbuki.
14. Na wanapo
ona Ishara, wanafanya maskhara.
15. Na husema:
Haya si chochote ila ni uchawi tu ulio dhaahiri.
16. Ati tukisha
kufa na tukawa udongo na mifupa ndio kweli tutafufuliwa?
17. Hata baba zetu wa zamani?
18. Sema: Naam! Hali nanyi ni madhalili.
19. Huko utapigwa ukelele mmoja tu! Na hapo ndio wataona!
20. Watasema: Ole wetu! Hii ndiyo Siku ya Malipo.
21. Hii ndiyo Siku ya Hukumu mliyo kuwa mkiikadhibisha.
22. Wakusanyeni walio dhulumu, na wake zao, na hao walio
kuwa wakiwaabudu -
23. Badala ya Mwenyezi Mungu. Waongozeni njia ya Jahannamu!
24. Na wasimamisheni. Hakika hao watasailiwa:
25. Mna nini? Mbona hamsaidiani?
26. Bali hii leo, watasalimu amri.
27.
Watakabiliana wao kwa wao kuulizana.
28.
Watasema: Kwa hakika nyinyi mlikuwa mkitujia upande wa kulia.
29.
Watasema (wakubwa): Bali nyinyi wenyewe hamkuwa Waumini.
30. Sisi
hatukuwa na mamlaka juu yenu, bali nyinyi wenyewe mlikuwa wapotovu.
31. Basi
hukumu ya Mola wetu Mlezi imekwisha tuthibitikia. Hakika bila ya shaka tutaonja
tu adhabu.
32.
Tulikupotezeni kwa sababu sisi wenyewe tulikuwa wapotovu.
33. Basi
wao kwa hakika siku hiyo watashirikiana katika adhabu pamoja.
34. Hivyo
ndivyo tutakavyo wafanyia wakosefu.
35. Wao
walipo kuwa wakiambiwa La ilaha illa 'Llahu Hapana mungu ila Mwenyezi Mungu tu,
wakijivuna.
36. Na
wakisema: Hivyo sisi tuiache miungu yetu kwa ajili ya huyu mtunga mashairi
mwendawazimu?
37. Bali
huyu amekuja kwa Haki, na amewasadikisha Mitume.
38. Hakika
nyinyi bila ya shaka mtaionja adhabu chungu.
39. Wala
hamlipwi ila hayo mliyo kuwa mkiyafanya.
40. Isipo
kuwa waja wa Mwenyezi Mungu walio khitariwa.
41. Hao ndio watakao pata riziki maalumu,
42.
Matunda, nao watahishimiwa.
43. Katika
Bustani za neema.
44. Wako
juu ya viti wamekabiliana.
45.
Wanazungushiwa kikombe chenye kinywaji cha chemchem
46.
Kinywaji cheupe, kitamu kwa wanywao.
47. Hakina
madhara, wala hakiwaleweshi.
48. Na
watakuwa nao wanawake wenye macho ya staha mazuri.
49. Hao
wanawake kama mayai yaliyo hifadhika.
50.
Waingie kuulizana wenyewe kwa wenyewe.
|