1 - 50
1. H'a Mim
2. Naapa
kwa Kitabu kinacho bainisha.
3. Hakika
Sisi tumeifanya Qur'ani kwa Kiarabu ili mfahamu.
4. Na
hakika hiyo imo katika Asili ya Maandiko yalioko kwetu, ni tukufu na yenye
hikima.
5. Je!
Tuache kukukumbusheni kabisa kwa kuwa nyinyi ni watu mlio pita mipaka kwa
ukafiri?
6. Na Manabii
wangapi tuliwatuma kwa watu wa zamani!
7. Na
hawajii Nabii yeyote ila walikuwa wakimkejeli.
8. Na
tuliwaangamiza walio kuwa na nguvu kushinda wao. Na mfano wa watu wa zamani
umekwisha pita.
9. Na
ukiwauliza: Nani aliye ziumba mbingu na ardhi? Bila ya shaka watasema: Kaziumba
Mwenye nguvu, Mjuzi,
10. Ambaye
amekufanyieni ardhi kama tandiko, na akakufanyieni ndani yake njia mpate
kuongoka.
11. Na
ambaye ndiye aliye teremsha kutoka mbinguni maji kwa kiasi, na kwa hayo tukaifufua
nchi iliyo kufa. Na namna hivi ndivyo mtakavyo tolewa.
12. Na
ambaye ndiye aliye umba katika kila kitu jike na dume, na akakufanyieni
marikebu na wanyama mnao wapanda.
13. Ili
mkae vizuri migongoni mwao, kisha mkumbuke neema za Mola wenu Mlezi mnapokaa
sawa sawa juu yao na mseme: Ametakasika aliye mfanya huyu atutumikie, na
tusingeli weza kufanya haya wenyewe.
14. Na hakika sisi tutarudi kwa Mola wetu Mlezi.
15. Na wanamfanyia katika waja wake fungu. Kwa hakika
mwanaadamu ni mtovu wa fadhila aliye dhaahiri.
16. Au amejichukulia watoto wanawake katika vile alivyo
viumba, na akakuteulieni nyinyi watoto wanaume?
17. Na anapo bashiriwa mmoja wao kwa yale aliyo mpigia
mfano Mwenyezi Mungu, uso wake husawijika na hujaa hasira.
18. Ati aliye lelewa katika mapambo, na katika mabishano
hawezi kusema kwa bayana...?
19. Na wakawafanya Malaika, ambao ni waja wa Mwingi wa
Rehema, ni wanawake! Kwani wameshuhudia kuumbwa kwao? Ushahidi wao utaandikwa
na wao watahojiwa!
20. Nao husema: Angeli penda Mwingi wa Rehema tusingeli
waabudu sisi. Hawana ujuzi
wowote wa hayo! Hawana ila kusema uwongo tu!
21. Kwani tuliwapa Kitabu kabla ya hichi, na ikawa wao
wanakishikilia hicho?
22. Bali wanasema: Hakika sisi tuliwakuta baba zetu
wanashika dini makhsusi, basi na sisi tunaongoza nyayo zao.
23. Na kadhaalika hatukumtuma mwonyaji kwenye mji wowote
ila watu wake walio deka kwa starehe walisema: Hakika sisi tuliwakuta baba zetu
wanashika dini makhsusi, na sisi tunafuata nyayo zao.
24. Akasema (Mwonyaji): Hata nikikuleteeni yenye uwongofu
bora kuliko mlio wakuta nao baba zenu? Wakasema: Sisi tunayakataa tu hayo mliyo
tumwa.
25. Basi tukawalipizia. Angalia ulikuwaje mwisho wa walio
kadhibisha!
26. Na pale Ibrahim alipo mwambia baba yake na kaumu yake:
Hakika mimi ninajitenga mbali na hayo mnayo yaabudu,
27. Isipo kuwa yule aliye niumba, kwani Yeye ataniongoa.
28. Na akalifanya hili liwe neno lenye kubaki katika vizazi
vyake ili warejee.
29. Bali tuliwastarehesha hawa na baba zao mpaka ikawafikia
Haki na Mtume aliye bainisha.
30. Na ilipo wafikia Haki wakasema: Huu ni uchawi, na sisi
hakika tunaukataa.
31. Na walisema: Kwa nini Qur'ani hii haikuteremshwa kwa
mtu mkubwa katika miji miwili hii?
32. Kwani wao ndio wanao gawa rehema za Mola wako Mlezi?
Sisi tumewagawanyia baina yao maisha yao katika uhai wa duniani, na
tukawanyanyua baadhi yao juu ya wengine kwa daraja nyingi; kwa hivyo baadhi yao
wanawafanya wenginewe wawatumikie. Na rehema za Mwenyezi Mungu ni bora kuliko
hayo wanayo yakusanya.
33. Na lau isinge kuwa watu watakuwa kundi moja tungeli
wajaalia wanao mkufuru Rahmani wana nyumba zao zina dari ya fedha, na ngazi zao
pia wanazo pandia,
34. Na milango ya nyumba zao na vitanda wanavyo egemea juu
yake,
35. Na mapambo. Lakini hayo si chochote ila ni starehe ya
maisha ya dunia tu, na Akhera iliyoko kwa Mola wako Mlezi ni ya wenye
kumchamngu.
36. Anaye yafanyia upofu maneno ya Rahmani tunamwekea
Shet'ani kuwa ndiye rafiki yake.
37. Na hakika wao wanawazuilia Njia na wenyewe wanadhani
kuwa wameongoka.
38. Hata atakapo tujia atasema: Laiti ungeli kuwako baina
yangu na wewe kama umbali baina ya mashariki na magharibi. Rafiki mwovu mno
wewe!
39. Na kwa kuwa mlidhulumu, haitakufaeni kitu leo kwamba
nyinyi mnashirikiana katika adhabu.
40. Je! Unaweza kuwasikilizisha viziwi, au unaweza
kuwaongoa vipofu na waliomo katika upotofu ulio wazi?
41. Na hata tukikuondoa, Sisi tutalipiza kisasi chetu kwao.
42. Au tutakuonyesha tulio waahidi. Nasi bila ya shaka tuna
uweza juu yao.
43. Basi wewe yashike yaliyo funuliwa kwako. Hakika wewe
uko kwenye Njia Iliyo Nyooka.
44. Na hakika haya ni ukumbusho kwako na kwa kaumu yako. Na
mtakuja ulizwa.
45. Na waulize Mitume wetu tulio watuma kabla yako: Je!
Tulifanya miungu mingine iabudiwe badala ya Rah'mani?
46, Na bila ya shaka tulimtuma Musa kwa Ishara zetu ende
kwa Firauni na waheshimiwa wake, na akasema: Hakika mimi ni Mtume wa Mola Mlezi
wa walimwengu wote!
47. Lakini alipo wajia na Ishara zetu wakaingia kuzicheka.
48. Na hatukuwaonyesha Ishara yoyote ila hiyo ilikuwa kubwa
zaidi kuliko nyenginewe. Na tukawakamata kwa adhabu ili warejee.
49. Na wakasema: Ewe mchawi! Tuombee kwa Mola wako Mlezi
kwa ile ahadi aliyo kuahidi; hakika sisi tutakuwa wenye kuongoka.
50. Basi tulipo waondolea adhabu hiyo, mara wakaingia kuvunja
ahadi.
|