53. SURAT ANNAJM
(Imeteremka
Makka)
Kiapo mwanzo wa Sura hii
kinadhihirisha ukweli wa Mtume s.a.w. katika anayo yasimulia ya khabari za
Wahyi (Ufunuo) na anayo yafikisha kutokana na huo ufunuo. Hakupoteza kitu
katika hayo wala hakukosea. Na Mtume s.a.w. amesema kweli katika aliyo
yazungumzia juu ya safari yake ya kwenda mbinguni, katika hayo yaliyo tokea ya
Miiraji, jicho lake halikuhangaika wala halikuruka mpaka.
Kisha Sura inaingia kueleza uchache wa akili za makafiri kwenda kuabudu
masanamu waliyo yaunda wenyewe kwa mikono yao, wakayaita majina yao wenyewe,
kama walivyo waita Malaika kuwa ati ni wanawake, baada ya kumfanya Mwenyezi
Mungu ana mabinti, na wao wenyewe wawe na watoto wa kiume.
Kisha Sura inamtaka Mtume s.a.w. awapuuze, na amwachilie mambo yao Mwenyezi
Mungu Mwenye kumiliki na kuumba vyote viliomo mbinguni na kwenye ardhi. Na Yeye
ndiye atakaye mlipa muovu kwa uovu wake, na mwema kwa wema wake. Naye ndiye
Mjuzi kabisa wa yote yanayo pita kwa viumbe vyake na hali zao. Yakafwatia hayo
kulaumiwa anaye kanya kuhisabiwa kila mtu kwa vitendo vyake, kama yalivyo
kwisha pita kwa sharia zilio tangulia, na ikasimuliwa na Vitabu vya Musa na
Ibrahim. Na Aya hizi zimethibitisha maana haya yaliyo elezwa katika uwezo na
Ishara za Mwenyezi Mungu katika mataifa yaliyo kwisha tangulia.
Kisha Sura inakhitimisha kwa kuweka wazi kwamba Qur'ani ni onyo miongoni mwa
maonyo walio onywa kwayo kaumu zilizo kwisha tangulia, ili wapate kutahadhari
na Siku ya Kiyama ambayo imekaribia wakati wake. Na Sura inawalaumu makafiri
wanao ikataa Qur'ani kwa kughafilika kwao huko, na wakawa wanacheka badala ya
kulia na kuwaidhika kwa Qur'ani. Na ikawataka Waumini wamsujudie Mwenyezi Mungu
aliye iteremsha na wamuabudu Yeye tu.
KWA JINA LA MWENYEZI
MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU
|