55. SURAT ARRAH'MAN
(Imeteremka
Madina)
Sura hii imeingia
kuzihisabu fadhila na neema za Mwenyezi Mungu, kwa kuanzia baada ya kumtaja
Arrah'man, Mwingi wa Rehema, kwa kutaja neema yake tukufu kabisa, nayo ni
Kufunza . Tena Aya zikaendelea kuzieleza hizo neema kwa namna ya kuweka wazi
utukufu wa Mwenye kuziumba, aliye tukuka shani yake; na inadhihirisha uweza
wake na ufalme wake juu ya wanaadamu na majini katika mbingu na ardhi.
Na inaeleza adhabu za wakosefu na wanao kadhibisha katika Jahannamu, na
ikafafanua neema za wachamngu Peponi.
Na Sura ikakhitimisha kwa kumtakasa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na kumsifu.
Na Sura imeikariri Aya isemayo "Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi
mnayo ikanusha?" mara thalathini na moja, katika mpango wa ki- Qur'ani
kukariri kunako pendeza kama inavyo wafikiana na haja. Kila moja katika hizo
Aya inawagonga hao wakanushaji kwa kuzikadhibisha kwao neema za Mwenyezi Mungu
katika Aya iliyo kabla yake.
KWA JINA LA MWENYEZI
MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU
|