1 - 50
1. Arrah'man, Mwingi wa Rehema
2. Amefundisha Qur'ani.
3. Amemuumba mwanaadamu,
4. Akamfundisha kubaini.
5. Jua na
mwezi huenda kwa hisabu.
6. Na
mimea yenye kutambaa, na miti, inanyenyekea.
7. Na mbingu ameziinua, na ameweka mizani,
8. Ili msidhulumu katika mizani.
9. Na wekeni mizani kwa haki, wala msipunje katika mizani.
10. Na ardhi ameiweka kwa ajili ya viumbe.
11. Humo yamo matunda na mitende yenye mafumba.
12. Na nafaka zenye makapi, na rehani.
13. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo
ikanusha
14. Amemuumba mtu kwa udongo wa kinamo..
15. Na akawaumba majini kwa ulimi wa moto.
16. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo
ikanusha
17. Mola Mlezi wa mashariki mbili na wa magharibi mbili.
18. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo
ikanusha?
19. Anaziendesha bahari mbili zikutane;
20. Baina yao kipo kizuizi, zisiingiliane.
21. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo
ikanusha?
22. Katika hizo bahari mbili zinatoka lulu na marijani.
23. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo
ikanusha?
24. Na ni vyake Yeye hivi viendavyo baharini vilivyo undwa
kama vilima.
25. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo
ikanusha?
26. Kila
kilioko juu yake kitatoweka.
27. Na
atabakia Mwenyewe Mola wako Mlezi Mwenye utukufu na ukarimu.
28. Basi
ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
29.
Vinamwomba Yeye vilivyomo katika mbingu na ardhi. Kila siku Yeye yumo katika
mambo.
30. Basi
ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
31. Tutakuhisabuni enyi makundi mawili.
32. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo
ikanusha?
33. Enyi makundi ya majini na watu! Mkiweza kupenya kwenye
mbingu na ardhi, basi penyeni! Hamtapenya ila kwa kupewa madaraka.
34. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo
ikanusha?
35. Mtapelekewa muwako wa moto na shaba; wala hamtashinda.
36. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo
ikanusha?
37. Itakapo pasuka mbingu ikawa nyekundu kama mafuta.
38. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo
ikanusha?
39. Siku hiyo hataulizwa dhambi zake mtu wala jini.
40. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
41. Watajuulikana wakosefu kwa alama zao, basi watashikwa
kwa nywele zao za utosini na kwa miguu.
42. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo
ikanusha?
43. Hii ndiyo Jahannamu ambayo wakosefu wakiikanusha.
44. Watakuwa wakizunguka baina ya hiyo na maji ya moto
yanayo chemka.
45. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo
ikanusha?
46. Na mwenye kuogopa kusimamishwa mbele ya Mola wake Mlezi
atapata Bustani mbili.
47. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo
ikanusha?
48. Bustani zenye matawi yaliyo tanda.
49. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo
ikanusha?
50. Ndani yake zimo chemchem mbili zinazo pita.
|