56. SURAT AL-WAAQIA'H
(Imeteremka
Makka)
Sura hii imeanzia kwa
kusimulia Tukio la Kiyama, na matokeo yatayo ambatana na Tukio hilo. Kisha
ikasimulia kuwa viumbe Siku hiyo watakuwa namna tatu. Ikafuatia hayo kwa
kufafanua kwa kutosha walio andaliwa kila fungu katika hao, ikiwa ni neema
zinazo wafikiana na cheo chao, au ni adhabu inayo nasibiana na ukafiri wao na
uasi wao.
Kisha Aya zikaweka wazi baada ya hayo yanayo onekana katika neema za Mwenyezi
Mungu Mtukufu, na athari za uweza wake katika viumbe, na makulima, na maji, na
moto; na yanayo hitajika kutokana na athari hizi kumsabihi Mwenyezi Mungu
Mtukufu na kumtakasa.
KWA JINA LA MWENYEZI
MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU
1. Litakapo tukia hilo Tukio
2. Hapana cha kukanusha kutukia kwake.
3. Literemshalo linyanyualo,
4. Itakapo tikiswa ardhi kwa mtikiso,
5. Na milima itapo sagwasagwa,
6. Iwe mavumbi yanayo peperushwa,
7. Na nyinyi mtakuwa namna tatu:-
8. Basi watakuwepo wa kuliani; je, ni wepi wa kuliani?
9. Na wa kushotoni; je, ni wepi wa kushotoni?
10. Na wa mbele
watakuwa mbele.
11. Hao
ndio watakao karibishwa
12. Katika
Bustani zenye neema.
13. Fungu kubwa
katika wa mwanzo,
14. Na wachache
katika wa mwisho.
15. Watakuwa juu
ya viti vya fakhari vilivyo tonewa.
16.
Wakiviegemea wakielekeana.
17.
Wakitumikiwa na wavulana wa ujana wa milele,
18. Kwa
vikombe na mabirika na bilauri za vinywaji kutoka chemchem safi.
19.
Hawataumwa kichwa kwa vinywaji hivyo wala hawatoleweshwa.
20. Na
matunda wayapendayo,
21. Na
nyama za ndege kama wanavyo tamani.
22. Na
Mahurulaini,
23. Walio
kama mfano wa lulu zilio hifadhiwa.
24. Ni
malipo kwa waliyo kuwa wakiyatenda.
25. Humo
hawatasikia porojo wala maneno ya dhambi,
26. Isipo kuwa maneno ya Salama, Salama.
27. Na wale wa mkono wa kulia, ni yepi yatakuwa ya wa
kuliani?
28. Katika mikunazi isiyo na miba, 29.
Na migomba iliyo pangiliwa,
30. Na kivuli kilicho tanda, 31.
Na maji yanayo miminika,
32. Na matunda mengi,
33. Hayatindikii wala hayakatazwi,
34. Na matandiko yaliyo nyanyuliwa.
35. Hakika Sisi tutawaumba (Mahurulaini) upya,
36. Na tutawafanya vijana,
37.
Wanapendana na waume zao, hirimu moja.
38. Kwa
ajili ya watu wa kuliani.
39. Fungu kubwa
katika wa mwanzo,
40. Na fungu
kubwa katika wa mwisho. 3
41. Na watu wa
kushotoni; je ni yepi ya wa kushotoni?
42. Katika upepo
wa moto, na maji yanayo chemka,
43. Na kivuli cha moshi mweusi,
44. Si cha kuburudisha wala kustarehesha.
45. Hakika hao walikuwa kabla ya haya wakiishi maisha ya
anasa.
46. Na walikuwa wakishikilia kufanya madhambi makubwa, 47.
Na walikuwa wakisema: Tutakapo kufa na tukawa udongo na mafupa, ati ndio
tutafufuliwa?
48. Au baba zetu
wa zamani?
49. Sema: Hakika wa zamani na wa mwisho
50. Bila ya shaka watakusanywa kwa wakati wa siku maalumu.
|