51 - 100
51. Kisha nyinyi, mlio potea, mnao kanusha,
52. Kwa yakini mtakula mti wa Zaqqumu.
53. Na kwa mti huo mtajaza matumbo.
54. Na juu yake mtakunywa maji yanayo chemka.
55. Tena mtakunywa kama wanavyo kunywa ngamia wenye kiu.
56. Hiyo ndiyo karamu yao Siku ya Malipo.
57. Sisi tumekuumbeni; basi hamsadiki?
58. Je! Mnaiona mbegu ya uzazi mnayo idondokeza?
59. Je! Mnaiumba nyinyi, au ni Sisi ndio Waumbaji?
60. Sisi tumekuwekeeni mauti; na wala Sisi hatushindwi 61.
Kuwaleta wengine badala yenu na kukuumbeni nyinyi kwa umbo msilo lijua.
62. Na bila ya shaka mlikwisha jua umbo la kwanza, basi kwa
nini hamkumbuki?
63. Je! Mnaona makulima mnayo yapanda?
64. Je! Ni nyinyi mnayo yaotesha au ni Sisi ndio wenye
kuotesha?
65. Tungeli taka tungeli yafanya yakawa mapepe, mkabaki
mnastaajabu,
66. Mkisema: Hakika sisi tumegharimika;
67. Bali sisi tumenyimwa.
68. Je! Mnayaona maji mnayo yanywa?
69. Je! Ni nyinyi mnayo yateremsha kutoka mawinguni au ni
Sisi ndio wenye kuyateremsha?
70. Tungeli penda tungeli yafanya ya chumvi. Basi mbona
hamshukuru?
71. Je! Mnauona moto mnao uwasha?
72. Ni nyinyi mlio uumba mti wake au Sisi ndio Waumbaji?
73. Sisi tumeufanya uwe ni ukumbusho na manufaa kwa walioko
nyikani.
74. Basi litakase jina la Mola wako Mlezi aliye Mkuu.
75. Basi naapa kwa maanguko ya nyota,
76. Na hakika bila ya shaka hichi ni kiapo kikubwa, laiti
mngeli jua!
77. Hakika
hii bila ya shaka ni ,
78. Katika
Kitabu kilicho hifadhiwa.
79. Hapana
akigusaye ila walio takaswa.
80. Ni
uteremsho unao toka kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote.
81. Ni
maneno haya ndiyo nyinyi mnayapuuza?
82. Na
badala ya kushukuru kwa riziki yenu mnafanya kuwa mnakadhibisha?
83. Yawaje
basi itakapo fika roho kwenye koo,
84. Na
nyinyi wakati huo mnatazama!
85. Na
Sisi tuko karibu zaidi naye kuliko nyinyi.
86. Na lau
kuwa nyinyi hamumo katika mamlaka yangu,
87.
Kwanini hamuirudishi hiyo roho, ikiwa nyinyi mnasema kweli?
88. Basi akiwa miongoni mwa walio karibishwa,
89. Basi ni raha, na manukato, na Bustani zenye neema.
90. Na akiwa katika watu wa upande wa kulia,
91. Basi ni Salamu kwako uliye miongoni mwa watu wa upande
wa kulia.
92. Na ama akiwa katika walio kadhibisha wapotovu,
93. Basi karamu yake ni maji yanayo chemka,
94. Na kutiwa Motoni.
95. Hakika hii ndiyo haki yenye yakini.
96. Basi litakase jina la Mola wako Mlezi aliye Mkubwa.
|