Table of Contents | Words: Alphabetical - Frequency - Inverse - Length - Statistics | Help | IntraText Library

Qu'rani

IntraText CT - Text

  • 93. SURAT WADH-DHUH'AA
Previous - Next

Click here to hide the links to concordance

93. SURAT WADH-DHUH'AA

(Imeteremka Makka)

Sura hii imeanza kwa viapo viwili vyenye kueleza nyakati mbili za uchangamfu na za kutulia, ya kwamba kwa hakika Mwenyezi Mungu hakumwacha Mtume wake wala hakumchukia, na kwamba aliyo mtengenezea katika Akhera makao ya juu ni bora zaidi kuliko alio mkirimu duniani. Kisha Subhanahu akaapa kwamba Yeye atampa mpaka aridhike, na yaliyo tangulia ni ushahidi wa yatakayo kuja. Kwani alikuwa yatima, akampatia makaazi; alikuwa amepotea akampa bora ya uwongofu, na alikuwa fakiri akamtajirisha. Kisha Aya zikataka aangaliwe vyema yatima, na asikemewe mwenye kuomba au kuuliza, na zisimuliwe neema za Mwenyezi Mungu.

KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

1. Naapa kwa mchana!

2. Na kwa usiku unapo tanda!

3. Mola wako Mlezi hakukuacha, wala hakukasirika nawe.

4. Na bila ya shaka wakati ujao utakuwa bora kwako kuliko ulio tangulia.

5. Na Mola wako Mlezi atakupa mpaka uridhike.

6. Kwani hakukukuta yatima akakupa makaazi?

7. Na akakukuta umepotea akakuongoa?

8. Akakukuta mhitaji akakutosheleza?

9. Basi yatima usimwonee!

10. Na anaye omba au kuuliza usimkaripie!

11. Na neema za Mola wako Mlezi zisimlie.

 




Previous - Next

Table of Contents | Words: Alphabetical - Frequency - Inverse - Length - Statistics | Help | IntraText Library

Best viewed with any browser at 800x600 or 768x1024 on Tablet PC
IntraText® (V89) - Some rights reserved by EuloTech SRL - 1996-2007. Content in this page is licensed under a Creative Commons License