Table of Contents | Words: Alphabetical - Frequency - Inverse - Length - Statistics | Help | IntraText Library

Qu'rani

IntraText CT - Text

  • 101. AL-QAARIA'H
Previous - Next

Click here to hide the links to concordance

101. AL-QAARIA'H

(Imeteremka Makka)

Sura hii inaanza kwa kitisho cha hiyo AL-QAARIA'H, yaani Inayo gonga, sauti inayo gonga katika masikio ya watu, yaani ndio Kiyama. Na Sura imetaja baadhi ya hali za hiyo sauti inayo gonga khasa kwa mintarafu ya watu na milima. Na ikashughulikia kusimulia hao ambao mizani yao itakuwa nzito kwa kuzidi mema yao, na mizani yao itayo kuwa duni kwa kuzidi maovu yao (na kupunguka mema yao).

KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

1. Inayo gonga!

2. Nini Inayo gonga?

3. Na nini kitacho kujuilisha nini Inayo gonga?

4. Siku ambayo watu watakuwa kama nondo walio tawanyika;

5. Na milima itakuwa kama sufi zilizo chambuliwa!

6. Basi yule ambaye mizani yake itakuwa nzito,

7. Huyo atakuwa katika maisha ya kupendeza.

8. Na yule ambaye mizani yake itakuwa khafifu,

9. Huyo maskani yake yatakuwa Moto wa Hawiya!

10. Na nini kitacho kujuilisha nini hiyo?

11. Ni Moto mkali!

 




Previous - Next

Table of Contents | Words: Alphabetical - Frequency - Inverse - Length - Statistics | Help | IntraText Library

Best viewed with any browser at 800x600 or 768x1024 on Tablet PC
IntraText® (V89) - Some rights reserved by EuloTech SRL - 1996-2007. Content in this page is licensed under a Creative Commons License