3. SURAT AL I'MRAN
(Imeteremka
Madina)
MIONGONI mwa mambo inayo
yazungumzia Qur'ani ni hadithi za ada ya Mwenyezi Mungu katika uumbaji wake, na
mifano na mazingatio yanayo patikana katika hizo hadithi. Na hubainisha katika
hadithi hizo mambo mengi yaliyo khusu itikadi, hukumu za sharia na nyendo
njema. Katika Sura iliyo pita yametajwa mfano wa mwendo wa Wana wa Israili.
Yameelezwa mengi ya walivyo kengeuka. Na katika Sura hii yanatajwa mengine ya
upotovu wao na kukengeuka kwao, na vipi Muumini anatakikana aongoke katika
itikadi yake na mwenendo wake, na pia unabainishwa humu ukweli wa Dini ya
Mbinguni, na inaonyeshwa vipi ziwe adabu za kujadiliana, na zinaelezwa ada za
wakati wa kushinda na pengine wakati wa kushindwa. Pia inabainishwa vipi
watakuwa wanao kufa Mashahidi Siku ya Kiyama, na yepi malipo yao. Na hayo yote
kwa wanaume na wanawake. Na inaelezwa kadhaalika njia ya mafanikio. Sura
hii tukufu inaanza kama ilivyo anza iliyo tangulia.
KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU
|