Table of Contents | Words: Alphabetical - Frequency - Inverse - Length - Statistics | Help | IntraText Library

Qu'rani

IntraText CT - Text

  • 5. SURAT AL MAIDA
Previous - Next

Click here to hide the links to concordance

5. SURAT AL MAIDA

(Imeteremka Madina)

Hii Sura ya Madina. Idadi za Aya zake ni 120. Na hii ni katika Sura zilizo shuka karibu na mwisho. Humu umebainishwa waajibu wa kutimiza maagano, sawa yakiwa baina ya mja na Mola wake Mlezi, au baina ya watu wenyewe kwa wenyewe. Na Sura hii imebainisha baadhi ya vyakula vilivyo harimishwa, kama ilivyo bainisha vilivyo halali, na kuhalalisha kuwaoa wanawake wa Ahlil Kitabi, Wakristo na Mayahudi. Zimetajwa pia humu nguzo za udhu na kutayamamu. Kadhaalika imeelezwa kutakikana kufanya uadilifu na adui. Na Sura hii imeashiria neema za Mwenyezi Mungu juu ya Waislamu, na waajibu wao kukihifadhi Kitabu chao, na ikaelezea kuwa Mayahudi wameyatengua maneno kutokana na pahala pake, na Wakristo wakayasahau baadhi ya mambo waliyo kumbushwa, na kwamba wao wamekufuru kwa kusema kwao kuwa Masihi ni mwana wa Mungu. Kadhaalika Sura hii inawakanusha Mayahudi na Wakristo kwa yale madai yao kwamba ati wao ni wana wa Mungu na vipenzi vyake. Kisha tena Sura hii imekusanya baadhi ya khabari za Mayahudi, kama ilivyo kusanya kisa cha wana wawili wa Adam. Kisa hichi kinathibitisha kuwa uvamizi na kudhulumiana ni katika tabia za kibinaadamu. Tena kuwajibika kumtoza kisasi mwenye kudhulumu ni njia ya kuidhibiti tabia hii mbovu isivuke mpaka! Na Sura Al Maidah imeeleza adhabu ya kumtia adabu mwenye kufanya fiski na wizi. Tena baadae ikarejea kubainisha vipi Mayahudi walivyo pindua hukumu za sharia zilizo kuwamo katika Taurati, na ikabainisha kwamba katika Taurati na Injili ulikuwapo ukweli na haki kabla ya kuchezewa na kugeuzwa geuzwa. Na ikahakikishwa kuwa ni waajibu kuhukumu kwa mujibu alivyo teremsha Mwenyezi Mungu. Sura imeashiria juu ya uadui wa Mayahudi na Wakristo kwa Waumini, na waajibu wa kutowanyenyekea, na kutowaridhia kwa wanayo tenda, na kuwa ni dharura kuwapinga. Na Sura imethibitisha kuwa Wakristo wamekufuru kwa kusema kwao Mwenyezi Mungu ni mmoja wa Watatu! Tena Qur'an katika Sura hii imewasifu baadhi ya Wakristo ambao wameikubali haki na wakaiamini, na ikamkataza Muumini kujiharimishia mwenyewe vitu vizuri, na ikabainisha nini kafara ya kuvunja kiapo. Sura hii kadhaalika imeharimisha ulevi kabisa, na imebainisha ibada za Hija na cheo cha Alkaaba na miezi mitakatifu, na ikaeleza upotovu wa baadhi ya mambo waliyo jiharimishia Waarabu wenyewe kwa wenyewe bila ya hoja wala dalili yoyote, kama ilivyo bainisha wasia wakati wa safari. Mwishoe Sura hii imekhitimisha kwa kutaja miujiza iliyo tokea kwa Nabii Isa a.s. Na juu ya hiyo miujiza Banu Israili walimkanya. Pia Sura imetaja kuwa Nabii Isa a.s. hana dhambi ya walio potoka wakamuabudu, na imeeleza Ufalme wa Mwenyezi Mungu Subhanahu juu ya mbingu na ardhi, na ukamilifu wa uwezo wake.

KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU, MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU.




Previous - Next

Table of Contents | Words: Alphabetical - Frequency - Inverse - Length - Statistics | Help | IntraText Library

Best viewed with any browser at 800x600 or 768x1024 on Tablet PC
IntraText® (V89) - Some rights reserved by EuloTech SRL - 1996-2007. Content in this page is licensed under a Creative Commons License