8. SURAT AL-ANFAAL
(Imeteremka
Madina)
Surat
Al Anfaal hii imeteremka Madina. Aya zake ni 75. Mwenyezi Mungu aliye takasika
na kutukuka, amebainisha katika Sura hii baadhi ya hukumu za vita, na mambo
yanayo pelekea vita, na sababu za ushindi, na makamo ya nguvu za moyo zinazo
pelekea kushinda, na hukumu za ngawira za vita, na wakati gani kuchukua mateka.
Na Mwenyezi Mungu kwa hikima yake amekusanya humu hukumu za kisharia. Sura hii
inaeleza kisa cha Vita vya Badri, na baadhi ya yaliyo kuwa kabla yake, na
kuashiria sababu zilizo sabibisha hivyo vita, nazo ni kutoka makafiri
washirikina Makka kumwendea Nabii s.a.w.. Na humu Mwenyezi Mungu anataja
kujitayarisha kwa vita, na kupasa kuelekea salama na amani ikiwa maadui wanaelekea
kutaka salama. Na Sura hii tukufu inamalizikia kubainisha urafiki wa Waumini,
wao kwa wao; na kuwawajibikia Waumini kuihama nchi inayo waonea na kuwafanya
wanyonge, ili wende kuwaunga mkono Waumini wenzao katika juhudi ya kutukuza
Uislamu na Waislamu.
KWA JINA LA MWENYEZI
MUNGU MWINGI WA REHEMA, MWENYE KUREHEMU
|