Table of Contents | Words: Alphabetical - Frequency - Inverse - Length - Statistics | Help | IntraText Library |
Qu'rani IntraText CT - Text |
|
|
1. SURAT AL-FAATIH'A (Imeteremka Makka) Sura
hii iliteremka Makka kabla ya Hijra, kuhamia Mtume s.a.w. Madina. Imeitwa
Al-Faatih'a, yaani Kifungulio kwa kuwa ndiyo sura ya mwanzo katika mpango wa
Msahafu Mtukufu, nayo ni sura ya mwanzo iliyo teremka kwa utimilivu wake. Na
sura hii inakusanya jumla ya yaliyomo katika Qur'ani na kama kwamba huu ni
mukhtasari wake, na baadaye yatakuja mambo kwa tafsili, babu-babu. 1. KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU. 2. Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote; 3. Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu; 4. Mwenye Kumiliki Siku ya Malipo. 5. Wewe tu tunakuabudu, na Wewe tu tunakuomba msaada. 6. Tuongoe njia iliyo nyooka, 7. Njia ya ulio waneemesha, siyo ya walio kasirikiwa, wala walio potea.
|
Table of Contents | Words: Alphabetical - Frequency - Inverse - Length - Statistics | Help | IntraText Library |
Best viewed with any browser at 800x600 or 768x1024 on Tablet PC IntraText® (V89) - Some rights reserved by EuloTech SRL - 1996-2007. Content in this page is licensed under a Creative Commons License |