Table of Contents | Words: Alphabetical - Frequency - Inverse - Length - Statistics | Help | IntraText Library |
Qu'rani IntraText CT - Text |
|
|
10. SURAT YUNUS (Imeteremka Makka) Sura hii ya Makka imeteremka Makka, na ina Aya 109. Imeanzia kuashiria cheo cha Kitabu hiki Kitukufu, na wasemayo washirikina yaliyo mkhusu Nabii s.a.w. Kisha ikataja ulimwengu na ishara za Mwenyezi Mungu Mtukufu ziliomo humo, na malipo ya Siku ya Kiyama, na mwendo wa Mwenyezi Mungu Mtukufu kuwatendea makafiri, na kuwakemea kwake kwa hizo itikadi zao, na hali ya watu wakati wa shida na neema, na uwezo wa Mwenyezi Mungu juu ya kila kitu, na kuemewa masanamu kufanya lolote. Na katika Sura hii wanatakiwa kama wanaweza makafiri walete Sura japo moja ya kuzua. Na pia ndani yake kuna vitisho vikali vya adhabu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na hali za nafsi za watu, na vipi Mwenyezi Mungu anavyo vichunguza vitendo vyao. Kisha baada ya hayo ikaingia kumwondolea Nabii s.a.w. kuungulika kwake kwa ukafiri wao, pamoja na kutoa hoja ya kuwavunja kabisa, na ikampoza kwa kumtajia hadithi za Manabii wengine na kaumu zao. Ikaja hadithi ya Nuhu, na hadithi ya Musa na Harun na Firauni na Wana wa Israili; kisha ikaashiriwa hadithi ya Yunus, na kwa jina hilo Sura hii ikaitwa. Na mwisho ikaelekea Sura hii kubainisha mambo ya Mtume huyu ili kutimiza mawaidha na mazingatio. KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU
|
Table of Contents | Words: Alphabetical - Frequency - Inverse - Length - Statistics | Help | IntraText Library |
Best viewed with any browser at 800x600 or 768x1024 on Tablet PC IntraText® (V89) - Some rights reserved by EuloTech SRL - 1996-2007. Content in this page is licensed under a Creative Commons License |