1 - 50
1. Alif
Lam Ra. (A.L.R). Hizi ni Aya za Kitabu na Qur'ani inayo bainisha.
2. HUENDA
ikawa walio kufuru wakatamani wange kuwa Waislamu.
3. Waache
wale, na wastarehe, na iwazuge tamaa. Watakuja jua.
4. Na
hatukuuangamiza mji wowote ule ila ulikuwa na muda wake maalumu.
5.
Hawawezi watu wowote kuitangulia ajali yao, wala kuchelewa.
6. Na
walisema: Ewe uliyeteremshiwa Ukumbusho! Hakika wewe ni mwendawazimu.
7. Mbona
hutuletei Malaika ikiwa wewe ni miongoni mwa wasemao kweli?
8. Sisi hatuwateremshi
Malaika ila kwa sababu ya haki, na hapo hawatapewa muhula.
9. Hakika
Sisi ndio tulio teremsha Ukumbusho huu, na hakika Sisi ndio tutao ulinda.
10. Na
hakika tulikwisha watumia Mitume mataifa ya mwanzo.
11. Na
hakuwafikia Mtume ila walimkejeli.
12. Na
kama hivi ndivyo tunavyo ingiza katika nyoyo za wakosefu.
13.
Hawayaamini haya, na hali ya kuwa umekwisha wapitia mfano wa watu wa kale.
14. Na lau
tungeli wafungulia mlango wa mbingu, wakawa wanapanda,
15. Basi
wangeli sema: Macho yetu yamelevywa, bali sisi wenyewe tumerogwa.
16. Na
hakika tumeweka katika mbingu vituo vya sayari, na tumezipamba kwa wenye
kuangalia.
17. Na tumezilinda na kila shetani afukuzwaye.
18. Isipo kuwa mwenye kusikiliza kwa kuibia, naye hufuatwa
na kijinga cha moto kinacho onekana.
19. Na ardhi tumeitandaza na humo tumeweka milima, na
tumeotesha kila kitu kwa kiasi chake.
20. Na tumekujaalieni humo vitu vya maisha yenu, na ya hao
ambao nyinyi sio wenye kuwaruzuku.
21. Na hakuna chochote ila asili yake inatokana na Sisi;
wala hatukiteremshi ila kwa kipimo maalumu.
22. Na tunazipeleka pepo za kupandishia, na tunateremsha kutoka
mbinguni maji, kisha tukakunywesheni maji hayo. Wala si nyinyi mnayo yaweka.
23. Na Sisi ndio tunao huisha na tunao fisha. Na Sisi ndio
Warithi.
24. Na tunawajua walio tangulia katika nyinyi, na tunawajua
walio taakhari.
25. Na hakika Mola wako Mlezi ndiye atakaye wakusanya.
Hakika Yeye ni Mwenye hikima na Mjuzi.
26. Na tulimuumba mtu kwa udongo unao toa sauti, unao tokana
na matope yaliyo tiwa sura.
27. Na majini tuliwaumba kabla kwa moto wa upepo umoto.
28. Na Mola wako Mlezi alipo waambia Malaika: Hakika Mimi
nitamuumba mtu kwa udongo unao toa sauti, unao tokana na matope yaliyo tiwa
sura.
29. Basi nitakapo mkamilisha na nikampulizia roho yangu,
basi mumwangukie kumsujudia.
30. Basi Malaika wote pamoja walimsujudia,
31. Isipo kuwa Iblisi. Yeye alikataa kuwa pamoja na walio
sujudu.
32. (Mwenyezi Mungu) akasema: Ewe Iblisi! Una nini hata
hukuwa pamoja na walio sujudu?
33. Akasema: Haiwi mimi nimsujudie mtu uliye muumba kwa
udongo unao toa sauti, unao tokana na matope yenye sura.
34.(Mwenyezi Mungu) akasema: Basi toka humo, kwani hakika
wewe ni maluuni!
35. Na hakika juu yako ipo laana mpaka Siku ya Malipo.
36. Akasema (Iblisi): Mola wangu Mlezi! Nipe muhula mpaka
siku watapo fufuliwa.
37. (Mwenyezi Mungu) akasema: Hakika wewe ni katika walio
pewa muhula
38. Mpaka siku ya wakati maalumu.
39. Akasema: Mola wangu Mlezi! Ilivyo kuwa umenitia
makosani, basi nahakikisha nitawazaini hapa duniani na nitawapoteza wote,
40. Ila waja wako walio safika.
41. Akasema: Hii Njia ya kujia kwangu Iliyo Nyooka.
42. Hakika waja wangu, wewe hutakuwa na mamlaka juu yao,
isipo kuwa wale wapotofu walio kufuata.
43. Na bila shaka Jahannamu ndipo pahali pao walipo ahidiwa
wote.
44. Ina milango saba; na kwa kila mlango iko sehemu walio
tengewa.
45. Hakika wachamngu watakuwa katika Mabustani na chemchem.
46. (Wataambiwa:) Ingieni kwa salama na amani.
47. Na tutaondoa chuki iliyo kuwamo vifuani mwao, wawe
ndugu juu ya viti vya enzi wameelekeana.
48. Humo hayatawagusa machofu, wala hawatatolewa humo.
49. Waambie waja wangu ya kwamba Mimi ndiye Mwenye
kusamehe, Mwenye kurehemu.
50. Na kwamba adhabu yangu ndio adhabu iliyo chungu!
|