Table of Contents | Words: Alphabetical - Frequency - Inverse - Length - Statistics | Help | IntraText Library

Qu'rani

IntraText CT - Text

  • 18. SURA AL KAHF
Previous - Next

Click here to show the links to concordance

18. SURA AL KAHF

(Imeteremka Makka)

Sura hii ni ya Makka, isipo kuwa Aya 38, na Aya zinazo anzia 83 mpaka 101. Basi zimo Aya ishirini za Madina. Nayo imeanzia kwa kumhimidi Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa kuiteremsha , na kubainisha kuwa Qur'ani ni onyo na bishara. Ndani yake lipo onyo kwa wanao dai kuwa ati Mwenyezi Mungu ana mwana. Na humu imetajwa hamu kubwa aliyo nayo Nabii ya kutaka waamini wale anao waita kwenye mlingano wa Mwenyezi Mungu. Kisha kikatajwa kisa cha Ahlil Kahf, Watu wa Pangoni, walio lala usingizi kisha wakaamka baada ya kukaa katika pango lao muda wa miaka mia tatu na tena wakazidishiwa tisa. Na watu hao walikuwa Wakristo walio kuwa wakikimbia udhalimu wa mtawala wa Kirumi. Wakalala katika pango muda huo, kisha wakaamka ili kuwa ni ishara ya uweza wa Mwenyezi Mungu Mtukufu kufufua baada ya kufa.
Kisha baada ya hayo Mwenyezi Mungu akamuamrisha kusoma Qur'ani na aitumie kwa kuonya na kubashiri. Kisha imebainishwa hali ya watu wa Peponi na watu wa Motoni. Na Mwenyezi Mungu akapiga mifano ya watu wawili, mmoja tajiri anajitapa kwa mali yake na wanawe. Na wa pili anatafakhari kwa Mwenyezi Mungu wake. Na amebainisha Subhanahu kuwa ulinzi wake ndio wa Haki. Na tena Subhanahu ameeleza starehe ya duniani inayo pita, na neema ya daima au adhabu chungu ya Siku ya Kiyama. Tena Subhanahu ametaja hadithi ya Musa pamoja na Mja Mwema aliye pewa ilimu kutokana na Mwenyezi Mungu. Na katika kisa hichi inapatikana sura ya vipi mtu anaweza asijue mambo, hata akiwa Nabii Mtume katika Mitume imara - Ulul a'zmi - kwa kudra yake Mwenyezi Mungu, ila akiwa Yeye Mwenyezi Mungu akimjuulisha. Tena anatajwa Dhul-qarnaini na kufika kwake mashariki ya mbali, na alivyo jenga Ukuta. Kisha yatakayo kuwa Siku ya Kiyama, na malipo ya Waumini, na ilimu ya Mwenyezi Mungu na maneno yake yasiyo malizika. Na Sura ikakhitimishia kwa kueleza Njia ya Kumridhi Subhanahu.

KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU




Previous - Next

Table of Contents | Words: Alphabetical - Frequency - Inverse - Length - Statistics | Help | IntraText Library

Best viewed with any browser at 800x600 or 768x1024 on Tablet PC
IntraText® (V89) - Some rights reserved by EuloTech SRL - 1996-2007. Content in this page is licensed under a Creative Commons License