101 - 110
101. Wale ambao kwamba macho yao yalikuwa paziani
hayanikumbuki, na wakawa hawawezi kusikia.
102. Je, wanadhani walio kufuru ndio wawafanye waja wangu
ndio walinzi wao badala yangu Mimi? Hakika Sisi tumeiandaa Jahannamu iwe ndipo
mahala pa kuteremkia makafiri.
103. Sema: Je, tukutajieni wenye khasara mno katika vitendo
vyao?
104. Ni wale ambao juhudi yao katika maisha ya dunia
imepotea bure, nao wanadhani kwamba wanafanya kazi nzuri.
105. Hao ni wale walio zikanusha Ishara za Mola wao Mlezi
na kukutana naye. Kwa hivyo vitendo vyao vimepotea bure, na wala Siku ya Kiyama
hatutawathamini kitu.
106. Hiyo Jahannamu ni malipo yao kwa walivyo kufuru na
wakafanyia kejeli Ishara zangu na Mitume wangu.
107. Hakika wale walio amini na wakatenda mema mashukio yao
yatakuwa kwenye Pepo za Firdausi.
108. Watadumu humo; hawatataka kuondoka.
109. Sema: Lau kuwa bahari ndio wino kwa maneno ya Mola
wangu Mlezi, basi bahari ingeli malizika kabla ya kumalizika maneno ya Mola
wangu Mlezi, hata tungeli ileta mfano wa hiyo kuongezea.
110. Sema: Mimi ni mwanaadamu kama nyinyi. Ninaletewa Wahyi
kwamba Mungu wenu ni Mungu Mmoja. Mwenye kutaraji kukutana na Mola wake Mlezi
basi naatende vitendo vyema, wala asimshirikishe yeyote katika ibada ya Mola
wake Mlezi.
|