Table of Contents | Words: Alphabetical - Frequency - Inverse - Length - Statistics | Help | IntraText Library

Qu'rani

IntraText CT - Text

  • 19. SURAT MARYAM
Previous - Next

Click here to show the links to concordance

19. SURAT MARYAM

(Imeteremka Makka)

Hii ni Sura iliyo teremka Makka, na hamna Aya za Madina ila Aya 57 na 71. Hisabu ya Aya zake ni 98. Imeanzia kwa harufi moja moja kama Sura nyingi nyenginezo. Ndani ya Sura hii kipo kisa cha kuzaliwa Yahya bin Zakariya (Alayhima Ssalam). Zakariya alitamani mwana na hali kesha fikilia ukongwe na mkewe ni tasa. Na kimetajwa pia kisa cha Bibi Bikra Maryam (A.S.) na kumzaa kwake Masihi (A.S.). Kisha kikatajwa kisa cha Ibrahim (A.S) na Wito wake kulingania Upweke wa Mwenyezi Mungu, na alivyo mtaka babaake aache kuabudu masanamu, na majibizano yao yaliyo jiri kwa ajili ya masanamu, na madaraka ya Shet'ani.
Pia wameashiriwa Manabii wengine katika dhuriya za Ibrahim, nao Ismail na Is-haq na dhuriya wa Is-haq. Tena kikagusiwa kisa cha Idris (A.S.). Na tena Mwenyezi Mungu Subhanahu akataja khabari za walio fuatia wakaja baada ya Manabii, watu wat'iifu na wengine maasi. Na akataja kuwa Pepo ndiyo malipo ya Waumini, na Moto ni malipo ya makafiri, na akazitaja hali za makafiri katika Jahannamu. Na tena Subhanahu akagusia ya wapotovu wanao sema kwamba Mwenyezi Mungu ana mwana.
Na Subhanahu amebainisha cheo cha Qur'ani, na amewaonya makafiri, na amepiga mifano ya watavyo teketea wanao waasi Manabii. Na akaashiria kwamba hao wamepotea kabisa, hawakuacha hata ukumbusho.

KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU




Previous - Next

Table of Contents | Words: Alphabetical - Frequency - Inverse - Length - Statistics | Help | IntraText Library

Best viewed with any browser at 800x600 or 768x1024 on Tablet PC
IntraText® (V89) - Some rights reserved by EuloTech SRL - 1996-2007. Content in this page is licensed under a Creative Commons License