Table of Contents | Words: Alphabetical - Frequency - Inverse - Length - Statistics | Help | IntraText Library |
Qu'rani IntraText CT - Text |
|
|
21. SURATUL ANBIYAA (Imeteremka Makka) HII NI SURA iliyo teremka Makka baada ya Surat Ibrahim. Aya zake ni 112. Inabainisha kukaribia Kiyama na hali washirikina wameghafilika nacho. Nao walidai kuwa Mtume hatokuwa binaadamu, na pengine wakisema kuwa hii Qur'ani ni uchawi, na pengine kuwa ni mashairi, na pengine ni ndoto za ovyo ovyo. Na maonyo yapo mbele yao. Na Mitume wote hawakuwa ila ni wanaadamu tu kama Muhammad s.a.w., na walio watangulia kabla yao walisema uwongo kama walivyo sema uwongo Makureshi. Mwenyezi Mungu aliwajaalia ajali yao, kwani Yeye ni Mweza wa kuteketeza na kubakisha, na ni vyake Yeye vyote viliomo katika mbingu na ardhi. Na Malaika kila walipo wanamtakasa kwa kumsabihi Mwenyezi Mungu Mtukufu wala hawasiti. Na hakika kwenda sawa mbingu na ardhi ni dalili kuwa Muumba wake ni Mmoja, kwani lau kuwa wangeli shirikiana waumbaji mambo yangeli fisidika. Na Mitume wote wamekuja na amri ya kuabudiwa Mwenyezi Mungu peke yake. Wala hana mwana, wala asiseme yeyote kuwa yeye ni mungu pamoja na Mwenyezi Mungu. Wasemao hivyo malipo yao ni Jahannamu. Na Subhanahu kabainisha utukufu wa viumbe vyake, na ajabu za uumbaji wake wa mbingu na ardhi. Na akabainisha hali ya washirikina na makafiri. Naye Subhanahu wa Taa'la amenabihisha vipi Mwenyezi Mungu Mtukufu anavyo wahifadhi watu, na akaashiria Subhanahu nini malipo ya makafiri Siku ya Kiyama. Na akataja hadithi ya Musa na Harun pamoja na Firauni, na hadithi ya Ibrahim pamoja na kaumu yake, na alivyo mneemesha kwa dhuriya wema. Naye Subhanahu wa Taa'la ametaja hadithi ya Luut' na kaumu yake, na walivyo angamizwa, na hadithi ya Nuhu a.s. na ukafiri wa kaumu yake, na walivyo teketezwa isipo kuwa walio amini. Kisha Subhanahu wa Taa'la akaashiria hadithi za Sulaiman, na Daud, na Ayub, na Ismail, na Idris, na Dhulkifli, na Dhunnuun, na Maryamu. Na akataja khabari za Juj na Maajuj. Naye Subhanahu amebainisha vitendo vyema na matunda yake, na malipo watayo lipwa wenye kumchamngu na wakatenda mema, na hali yao Siku ya Kiyama, na rehema ya Mwenyezi Mungu katika Ujumbe wa Muhammad, na maonyo ya Mwenyezi Mungu kwa washirikina. Na kwamba hakika amri yote ni yake Yeye anavyo hukumu, na Yeye ndiye Mbora wa mahakimu. KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU
|
Table of Contents | Words: Alphabetical - Frequency - Inverse - Length - Statistics | Help | IntraText Library |
Best viewed with any browser at 800x600 or 768x1024 on Tablet PC IntraText® (V89) - Some rights reserved by EuloTech SRL - 1996-2007. Content in this page is licensed under a Creative Commons License |