Table of Contents | Words: Alphabetical - Frequency - Inverse - Length - Statistics | Help | IntraText Library |
Qu'rani IntraText CT - Text |
|
|
22. SURATUL HAJJ (Imeteremka Madina) Sura hii ni ya Madina ila Aya 52, 53, 54, na 55. Aya zake ni sabiini na nane. Imeanzia kwa kuwaonya watu wamkhofu Mwenyezi Mungu, na kukumbusha vitisho vya Kiyama, na kuwajuilisha wanao bisha kwa upotovu na ujinga, na hayo yakafuatia kuletwa dalili za kufufuliwa, kwa kuleta sura ya mabadiliko katika kuumbwa binaadamu na kukua kwa mimea, na ikaeleza upinzani kumpinga Mwenyezi Mungu, na matokeo yake. Na ikataja khabari ya Hija na kutukuza ibada zake. Na baada ya hayo Mwenyezi Mungu akaruhusu kupigana vita vya kujitetea. Na akafuatilizia hayo kumpoza Mtume s.a.w. kwa masaibu yaliyo kuwa yanampata kwa watu wake, kwa kutaja dhiki na mateso yaliyo wapata Mitume wa kabla yake. Na Aya za Sura hii zikabainisha dalili za uweza wake Mwenyezi Mungu Mtukufu na upweke wake, na mipaka ya kazi ya Mitume. Na kwamba hili ni onyo lisilo kimbilika. Na katika mwisho wa Sura wakasema hao wanao ambiwa ni washirika wa Mwenyezi Mungu kwa kuzizuga akili za washirikina, kwamba hawawezi hata kuumba kiumbe kinyonge kabisa, naye ni nzi. Na nzi akiwapokonya kitu hawawezi kukipata kwake. Na Sura ikahimiza Sala, na Zaka, na Ibada, na Jihadi, bila ya kukusudia maovu. Kwani hii ni Dini ya baba yenu Ibrahim aliye mzaa Ismail, ambaye kutokana naye ndio wakazalika ukoo wa A'dnan. Na matokeo ya mambo yenu ni kuwa Mtume wenu akushuhudieni kwa kukufikishieni Ujumbe, na nyinyi mtoe ushahidi juu ya watu walio kwisha tangulia kwamba Mitume wao waliwafikishia Ujumbe kama ilivyo kujieni katika Qur'ani. Na Sura ikakhitimisha kwa kutaka kushikamana na Mwenyezi Mungu. Kwani Yeye ndiye bora ya Mlinzi, na bora ya Mwenye kunusuru. KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU
|
Table of Contents | Words: Alphabetical - Frequency - Inverse - Length - Statistics | Help | IntraText Library |
Best viewed with any browser at 800x600 or 768x1024 on Tablet PC IntraText® (V89) - Some rights reserved by EuloTech SRL - 1996-2007. Content in this page is licensed under a Creative Commons License |