101 - 150
101. Wala rafiki wa dhati.
102. Laiti tungeli pata kurejea tena tungeli kuwa katika
Waumini.
103. Hakika katika haya ipo Ishara, lakini wengi wao
hawakuwa wenye kuamini.
104. Na hakika Mola wako Mlezi ndiye Mwenye nguvu Mwenye
kurehemu.
105. Kaumu ya Nuhu waliwakadhibisha Mitume.
106. Alipo waambia ndugu yao, Nuhu: Je! Hamchimngu?
107.
Hakika mimi kwenu ni Mtume muaminifu.
108. Basi Mcheni Mwenyezi Mungu, na nit'iini mimi.
109. Na sikutakini juu yake ujira, kwani ujira wangu hauko
ila kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote.
110. Basi Mcheni Mwenyezi Mungu, na nit'iini mimi.
111. Wakasema: Je! Tukuamini wewe, hali wanao kufuata ni
watu wa chini?
112. Akasema: Nayajuaje waliyo kuwa wakiyafanya?
113. Hisabu yao haiko ila kwa Mola wao Mlezi, laiti mngeli
tambua!
114. Wala mimi si wa kuwafukuza Waumini.
115. Mimi si cho chote ila ni Mwonyaji wa dhaahiri
shaahiri.
116. Wakasema: Ikiwa huachi, ewe Nuhu, bila ya shaka
utapigwa mawe.
117. Akasema: Mola wangu Mlezi! Hakika watu wangu wamenikanusha.
118. Basi hukumu baina yangu na wao kwa hukumu yako, na
uniokoe mimi na walio pamoja nami, Waumini.
119. Kwa hivyo tukamwokoa yeye na walio kuwa pamoja naye
katika marikebu iliyo sheheni.
120. Kisha tukawazamisha baadaye walio bakia.
121. Hakika katika haya ipo Ishara, lakini si wengi wao
walio kuwa Waumini.
122. Na hakika Mola wako Mlezi ndiye Yeye Mwenye nguvu
Mwenye kurehemu.
123. Kina A'd waliwakanusha Mitume.
124. Alipo waambia ndugu yao, Hud: Je! Hamchimngu?
125. Hakika
mimi kwenu ni Mtume muaminifu.
126. Basi mcheni Mwenyezi Mungu, na nit'iini mimi.
127. Wala sikutakeni juu yake ujira, kwani ujira wangu
hauko ila kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote.
128. Je! Mnajenga juu ya kila mnyanyuko kumbusho la
kufanyia upuuzi?
129. Na mnajenga majengo ya fakhari kama kwamba mtaishi
milele!
130. Na mnapo tumia nguvu mnatumia nguvu kwa ujabari.
131. Basi mcheni Mwenyezi Mungu, na nit'iini.
132. Na mcheni aliye kupeni haya mnayo yajua.
133. Amekupeni wanyama wa kufuga na wana.
134. Na mabustani na chemchem.
135. Hakika mimi ninakukhofieni adhabu ya Siku Kubwa.
136. Wakasema: Ni mamoja kwetu, ukitupa mawaidha au hukuwa
miongoni mwa watoao mawaidha.
137. Haya si chochote ila ni mtindo wa watu wa tokea
zamani.
138. Wala sisi hatutaadhibiwa.
139. Wakamkanusha; nasi tukawaangamiza. Hakika bila ya
shaka katika haya ipo Ishara. Lakini hawakuwa wengi wao wenye kuamini.
140. Na hakika Mola wako Mlezi ndiye Mwenye nguvu Mwenye
kurehemu.
141. Kina
Thamud waliwakanusha Mitume.
142. Alipo waambia ndugu yao Saleh: Je! Hamumchimngu?
143. Hakika mimi kwenu ni Mtume muaminifu.
144. Basi mcheni Mwenyezi Mungu, na nit'iini.
145. Wala sikutakini ujira juu yake. Ujira wangu hauko ila
kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote.
146. Je! Mtaachwa salama usalimina katika haya yaliyopo
hapa?
147. Katika mabustani, na chemchem?
148. Na konde na mitende yenye makole yaliyo wiva.
149. Na mnachonga milimani majumba kwa ustadi.
150. Basi mcheni Mwenyezi Mungu, na nit'iini mimi.
|