151 - 200
151 Wala msit'ii amri za walio pindukia mipaka,
152. Ambao wanafanya ufisadi katika nchi, wala
hawatengenezi.
153. Wakasema: Hakika wewe ni miongoni mwa walio rogwa.
154. Wewe si chochote ila ni mtu kama sisi. Basi lete
Ishara ukiwa wewe ni miongoni mwa wasemao kweli.
155. Akasema: Huyu ngamia jike; awe na zamu yake ya kunywa,
na nyinyi muwe na zamu yenu ya kunywa katika siku maalumu.
156. Wala msimguse kwa uwovu, isije ikakushikeni adhabu ya
Siku Kubwa.
157. Lakini wakamuuwa, na wakawa wenye kujuta.
158. Basi ikawapata adhabu. Hakika katika hayo ipo Ishara. Lakini hawakuwa wengi wao wenye kuamini.
159. Na hakika
Mola wako Mlezi ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu.
160. Watu wa
Lut'i waliwakanusha Mitume.
161. Alipo
waambia ndugu yao, Lut'i: Je! Hamumchimngu?
162. Hakika mimi
kwenu ni Mtume muaminifu kwenu.
163. Basi mcheni Mwenyezi Mungu na nit'iini mimi.
164. Wala mimi sikutakini ujira juu yake; ujira wangu hauko
ila kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote.
165. Je! Katika viumbe vyote mnawaingilia wanaume?
166. Na mnaacha alicho kuumbieni Mola wenu Mlezi katika
wake zenu? Ama kweli nyinyi ni watu mnao ruka mipaka!
167. Wakasema: Ewe Lut'i! Usipo acha, hapana shaka utakuwa
miongoni mwa wanao tolewa mji!
168. Akasema: Hakika mimi ni katika wanao kichukia hichi
kitendo chenu.
169. Mola wangu Mlezi! Niokoe mimi na ahali zangu na haya
wayatendayo.
170. Basi tukamwokoa yeye na ahali zake wote,
171. Isipo kuwa kikongwe katika walio kaa nyuma.
172. Kisha
tukawaangamiza wale wengine.
173. Na tukawanyeshea
mvua, basi ni ovu mno mvua ya waliyo onywa.
174.
Hakika katika hayo ipo Ishara. Na hawakuwa wengi wao wenye kuamini.
175. Na
hakika Mola wako Mlezi bila ya shaka ndiye Mwenye nguvu, Mwenye kurehemu.
176. Watu
wa Machakani waliwakanusha Mitume.
177.
Shuaibu alipo waambia: Je! Hamfanyi mkamchamngu?
178.
Hakika mimi kwenu ni Mtume muaminifu.
179. Basi mcheni Mwenyezi Mungu, na nit'iini mimi.
180. Wala sikutakini ujira juu yake. Ujira wangu hauko ila
kwa Mola Mlezi wa walimwengu wote.
181. Timizeni kipimo sawa sawa, wala msiwe katika wanao
punja.
182. Na pimeni kwa haki iliyo nyooka;
183. Wala msiwapunje watu vitu vyao, wala msifanye jeuri
kwa ufisadi.
184. Na mcheni aliye kuumbeni nyinyi na vizazi vilivyo
tangulia.
185. Wakasema: Hakika wewe ni katika walio rogwa.
186. Na wewe si chochote ila ni mtu tu kama sisi, na kwa
yakini tunakuona wewe ni katika waongo.
187. Hebu tuangushie vipande kutoka mbinguni ikiwa wewe ni
miongoni mwa wasemao kweli.
188. Akasema: Mola wangu Mlezi anajua zaidi mnayo yatenda.
189. Basi walimkanusha, na ikawashika adhabu ya siku ya
kivuli. Hakika hiyo ilikuwa adhabu ya siku kubwa.
190. Hakika katika hayo ipo Ishara, lakini hawakuwa wengi
wao wenye kuamini.
191. Na hakika Mola wako Mlezi bila ya shaka ndiye Yeye
Mwenye nguvu Mwenye kurehemu.
192. Na bila ya shaka hii ni Uteremsho wa Mola Mlezi wa
walimwengu wote.
193. Ameuteremsha Roho muaminifu,
194. Juu ya moyo wako, ili uwe katika Waonyaji,
195. Kwa ulimi wa Kiarabu ulio wazi.
196. Na hakika bila ya shaka haya yamo katika Vitabu vya
kale.
197. Je! Haikuwa kwao ni Ishara kwamba wanayajua haya
wanazuoni wa Wana wa Israili?
198. Na lau kuwa tungeli iteremsha juu ya mmoja wa wasio
kuwa Waarabu,
199. Na akawasomea, wasingeli kuwa wenye kuamini.
200. Namna hivi tunaingiza katika nyoyo za wakosefu.
|