Table of Contents | Words: Alphabetical - Frequency - Inverse - Length - Statistics | Help | IntraText Library |
Qu'rani IntraText CT - Text |
|
|
29. SURAT AL A'NKABUT (Imeteremka Makka) SURA HII NI ya Makka, na idadi ya Aya zake ni 69. Lakini Aya 1 mpaka 11 ziliteremka Madina. Sura hii imeanzia kwa kubainisha kwamba hapana budi ila Imani ya Waumini itiwe mitihanini kwa misukosuko na jihadi kwa ajili ya kulinda dola ya Haki na Imani. Na binaadamu ameusiwa kwa wazazi wake pamoja na amri ya jihadi, ili ukusanyike wema na jihadi, na baina ya watu wa namna mbali mbali na Imani. Na imeelezwa kwamba miongoni mwao yupo anaye sema kwa ulimi wake kwamba ameamini na hali moyo wake haukukubali. Kisha Sura hii imetaja khabari za Nuhu na kaumu yake, na kadhaalika imeeleza kisa cha Ibrahim katika wito wake. Na ikabainisha mafunzo hayo kwa ajili ya Mtume s.a.w. Kisha ikasimulia jawabu ya watu wa Ibrahim. Na ikaeleza khabari za Lut'i na kisa cha kaumu yake, na kuteremka kwa Wajumbe Malaika wa Mwenyezi Mungu kuja kuwahiliki, na wakaokoka ahali zake isipo kuwa mkewe. Kisha Subhanahu akaashiria kisa cha Shuaibu pamoja na Madyana, na cha Hud na A'di, na Saleh na Thamud, na kudanganyikiwa kwa Qaruni na Firauni na Hamani na matokeo ya mwisho wao. Na Yeye Subhanahu amebainisha kwamba kuabudu masanamu kwa washirikina kunategemea hoja iliyo kuwa dhaifu kabisa kuliko jumba la buibui. Na kwamba mifano kama hii hawaielewi ila wale wanao tumia akili zao. Na baada ya hayo Mwenyezi Mungu akamuamrisha Nabii wake asijadiliane na Watu wa Kitabu ila kwa njia nzuri. Na Yeye Subhanahu akaashiria kwamba Nabii s.a.w. hajui kusoma wala kuandika, na hayo yanazidi kuonyesha Utume wake. Na pia Subhanahu ametaja ukaidi wa washirikina katika kutaka kwao waletewe miujiza ya kuiona, nayo wataikataa kama walivyo ikataa kaumu ya Musa na wengineo. Na akagusia kule kuhimiza kwao kuteremshiwa adhabu. Naye amewabainishia adhabu itakayo wapata. Naye Subhanahu akataja malipo ya Waumini na Makafiri Siku ya Kiyama, na akataka watu watazame baada ya hayo ulimwengu na neema za Mwenyezi Mungu Mtukufu ziliomo ndani yake. Kisha akataja thamani ya uhai wa duniani ukilinganisha na wa Akhera, na hali ya washirikina katika unyonge wao na kumkimbilia kwao Mwenyezi Mungu wanapo kuwa katika khofu, na wanapo kuwa na nguvu na wakawa katika usalama wanavyo mshirikisha Mwenyezi Mungu. Kisha akaeleza neema zake anazo wapa katika Nyumba Takatifu ya Makka, na wanavyo zikanya neema hizo. Kisha Mwenyezi Mungu akabainisha fadhila za wanao pigana Jihadi. KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU
|
Table of Contents | Words: Alphabetical - Frequency - Inverse - Length - Statistics | Help | IntraText Library |
Best viewed with any browser at 800x600 or 768x1024 on Tablet PC IntraText® (V89) - Some rights reserved by EuloTech SRL - 1996-2007. Content in this page is licensed under a Creative Commons License |