51 - 60
51. Na tunge utuma upepo na wakauona umekuwa rangi ya
manjano, juu ya hayo wange endelea kukufuru.
52. Kwani wewe hakika huwafanyi maiti wakasikia, wala
viziwi wakasikia wito wakisha geuka kukupa mgongo.
53. Wala wewe huwaongoi vipofu na upotovu wao.
Huwasikilizishi ila wanao ziamini Aya zetu. Hao ndio Waislamu, walio nyenyekea.
54. Mwenyezi Mungu ndiye aliye kuumbeni kutokana na udhaifu
kisha akajaalia nguvu baada ya unyonge, kisha akajaalia baada ya nguvu unyonge
tena na ukongwe. Anaumba atakavyo. Naye ndiye Mjuzi, Mwenye uweza.
55. Na siku itapo simama Saa wakosefu wataapa kwamba
hawakukaa duniani ila saa moja tu. Hivyo ndivyo walivyo kuwa wakipotozwa.
56. Na walio pewa ilimu na Imani watasema: Hakika nyinyi
mlikwisha kaa katika hukumu ya Mwenyezi Mungu mpaka Siku ya kufufuliwa. Basi
hii ndiyo Siku ya kufufuliwa! Lakini nyinyi mlikuwa hamuijui.
57. Basi Siku hiyo hautawafaa walio dhulumu udhuru wao,
wala haitotakiwa toba yao.
58. Na hakika tulikwisha wapigia watu kila mfano katika hii
Qur'ani. Na ukiwaletea Ishara yoyote hapana shaka walio kufuru watasema: Nyinyi
si chochote ila ni waongo.
59. Hivi ndivyo Mwenyezi Mungu anavyo piga muhuri kwenye
nyoyo za wasio jua.
60. Basi subiri. Hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu ni ya haki.
Wala wasikupaparishe hao wasio
kuwa na yakini.
|