Table of Contents | Words: Alphabetical - Frequency - Inverse - Length - Statistics | Help | IntraText Library |
Qu'rani IntraText CT - Text |
|
|
33. SURAT AL-AH'ZAB (Imeteremka Madina) Sura hii imeanza kwa
kumtaka Mtume wa Mwenyezi Mungu s.a.w. amche Mwenyezi Mungu na amtegemee Yeye.
Tena ikaingia kuzungumza juu ya mas-ala ya watoto wa kupanga, na ikakataa kuwa
hao wana wanao walea kuwa ni watoto wao khasa. Na ikataja mapenzi na ut'iifu wa
Mwenyezi Mungu alio wajibisha kwa ajili ya Mtume wake, na hishima na kuwatukuza
Mamama wa Waumini, yaani wake za Mtume. Na Sura imeeleza ahadi aliyo ichukua
Mwenyezi Mungu kwa Manabii kuwa wafikishe ujumbe; na ikafafanua khabari za Vita
vya Ah'zab (Makundi) na khofu na misukosuko iliyo kuwako, na vipi mwishoe
Waumini wakashinda na ahadi ya Mwenyezi Mungu ikatimia. Na Sura hii
ikashughulikia kutaja adabu ambazo zinawapasa wake za Mtume kuzifuata, na
wajilazimishe nafsi zao kuzishika. Tena ikaangukia kuzungumza juu ya watoto wa
kupanga, na ikavunja ada ya siku za kijahiliya, za ujinga, ilipo kuwa
kuharimisha mtu kuoana na mwana wa kupanga ambaye kwa hakika ni halali yake. Na
Sura ikamsifu Mtume s.a.w. na ikamthibitishia aliyo kuwa anastahiki. Na ikausia
kustareheshwa na kumwacha kwa wema mwanamke anaye pewa talaka kabla ya kuingia
harusi. Na ikamkhusisha Mtume s.a.w. kuwa imemhalalishia mwanamke aliye jitolea
kuolewa naye, na ikasema wazi kuwa si halali kwake kuzidisha kuowa wanawake
wengine baada ya hao tisa alio kuwa nao. Kisha Sura tukufu ikabainisha yanayo
wajibikia Waumini kuyafuata wanapo ingia nyumba za Nabii kwa ajili ya kula, na
kuwa wakisha wende zao, na juu ya kuwauliza wake zake nyuma ya pazia. Na Sura
ikawataka Mamama wa Waumini (wake za Mtume s.a.w.) wateremshe mitandio yao juu
ya vifua vyao. Na Sura ikazungumza juu ya Saa na vitisho vya Kiyama, na ikatoa
nasaha ya kumcha Mwenyezi Mungu, na kusema maneno yaliyo sawa, na
ikakhitimishia kwa kutaja jukumu la Mwenyezi Mungu alilo libeba mwanaadamu,
hali mbingu na ardhi na milima ilishindwa kulibeba. KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU
|
Table of Contents | Words: Alphabetical - Frequency - Inverse - Length - Statistics | Help | IntraText Library |
Best viewed with any browser at 800x600 or 768x1024 on Tablet PC IntraText® (V89) - Some rights reserved by EuloTech SRL - 1996-2007. Content in this page is licensed under a Creative Commons License |