Table of Contents | Words: Alphabetical - Frequency - Inverse - Length - Statistics | Help | IntraText Library

Qu'rani

IntraText CT - Text

  • 36. SURAT YA-SIN
Previous - Next

Click here to show the links to concordance

36. SURAT YA-SIN

(Imeteremka Makka)

Sura hii imeanzia kwa harufi mbili ambazo ni katika harufi za kuundiwa maneno ya Kiarabu. Na ikafuatiliza kwa kuapa kwa Qur'ani ya kwamba Muhammad s.a.w. bila ya shaka ni miongoni mwa Mitume, walio tumwa. Na kuwa hakika yeye yuko kwenye Njia Iliyo Nyooka iliyo rasimiwa na Qur'ani aliyo teremshiwa yeye kutokana na Mtukufu Mwenye nguvu, Mwenye kurehemu, ili apate kuwaonya kwayo watu ambao baba zao hawakupata kabla yake kuonywa. Tena Sura ikaingia kutufanyia taswira, picha, ya wanao kataa, ambao hawanafiiki na maonyo. Na inatubainishia kwamba kuonya humfaidisha mwenye kuelekea kupokea makumbusho, na kumcha Mwingi wa Rehema. Na kwamba hakika Mwenyezi Mungu atawafufua wafu, na atavihisabu vitendo vya waja. Na Sura ikaingilia kuwapigia mfano makafiri wa Makka, na ikabainisha mvutano baina ya wanao mlingania Mwenyezi Mungu na wanao kadhibisha. Inabainisha mwisho wa makundi mawili hayo. Kisha ikawa inaeleza dalili za uweza unao pasa kuuamini na kuogopa miadi ya Mwenyezi Mungu itakayo watokea ghafla katika Siku ambayo kila mtu atalipwa kwa aliyo yatenda. Watu wa Peponi watastareheshwa. Watapata wanacho kitamani. Na watu wa Motoni watafukuzwa. Nao watakuwa katika mbano wa uweza wa Mwenyezi Mungu. Midomo yao itazibwa, na viungo vyao ndivyo vitavyo tamka. Na Mwenyezi Mungu angeli penda, basi bila ya shaka angeli zigeuza sura zao pia. Kwani ni Yeye ndiye Mwenye kumbadilisha anaye mrefushia umri wake duniani badala ya nguvu akawa dhaifu, na badala ya akili akawa amepiswa. Na Yeye ndiye aliye mlinda Nabii wake na kuzugwa na kichaa. Naye hakumfundisha utungaji mashairi, na wala hauhitajiki ufundi huo unao mfanya aliye nao kutanga tanga katika kila bonde. Mtume hakuja ila kwa ajili ya ukumbusho ulio wazi, ulio tokana na akili, sio ulio tokana na mawazo mapepe tu. Na Sura ikaendelea kukumbusha fadhila za Mwenyezi Mungu juu ya waja wake, na kwamba Yeye amewafanya wanyama wa mifugo ambao wanawamiliki na wanawapanda wawatumikie. Na juu ya neema hizi zilio wekwa kwa faida yao, wao bado wanakwenda kuabudu miungu ya ushirikina isiyo weza kitu. Na Sura inakhitimisha kwa kumtaka binaadamu aangalie namna alivyo umbwa kutokana na tone la manii, na khalafu yeye anakuwa ni mpinzani wa kudhihirisha upinzani wake. Na yule aliye umba hapo mwanzo, na anaye toa moto kutoka mti wa kijani, na aliye umba mbingu na ardhi, huyo basi ni Muweza wa kuyafufua mafupa nayo yamekwisha vurugika. Na amri yake ni kukiambia kitu: Kuwa! Na kikawa. Ametakasika Mwenye kumiliki kila kitu. Na kwake Yeye mtarejea.

KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU




Previous - Next

Table of Contents | Words: Alphabetical - Frequency - Inverse - Length - Statistics | Help | IntraText Library

Best viewed with any browser at 800x600 or 768x1024 on Tablet PC
IntraText® (V89) - Some rights reserved by EuloTech SRL - 1996-2007. Content in this page is licensed under a Creative Commons License