151 - 182
151. Ati ni kwa uzushi wao ndio wanasema:
152. Mwenyezi Mungu amezaa! Ama hakika bila ya shaka hao ni
waongo!
153. Ati amekhiari watoto wa kike kuliko wanaume?
154. Mna nini? Mnahukumu vipi nyinyi?
155.
Hamkumbuki?
156. Au
mnayo hoja iliyo wazi?
157. Basi
leteni Kitabu chenu kama mnasema kweli.
158. Na
wameweka makhusiano ya nasaba baina yake na majini; na majini wamekwisha jua
bila ya shaka kuwa wao watahudhurishwa.
159.
Subhana 'Llah Ametakasika Mwenyezi Mungu na hayo wanayo msingizia.
160. Isipo
kuwa waja wa Mwenyezi Mungu walio safishwa.
161. Basi
hakika nyinyi na mnao waabudu
162.
Hamwezi kuwapoteza
163. Isipo kuwa yule atakaye ingia Motoni.
164. Na hapana katika sisi ila anapo mahali pake maalumu.
165. Na hakika bila ya shaka sisi ndio wajipangao safu.
166. Na hakika sisi ndio wenye kusabihi kutakasa.
167. Na walikuwapo walio kuwa wakisema:
168. Tungeli kuwa na Ukumbusho kama wa watu wa zamani,
169. Bila ya shaka tungeli kuwa ni waja wa Mwenyezi Mungu
wenye ikhlasi.
170. Lakini waliukataa. Basi watakuja jua.
171. Na bila ya shaka neno letu lilikwisha tangulia kwa
waja wetu walio tumwa.
172. Ya kuwa wao bila ya shaka ndio watakao nusuriwa.
173. Na kwamba jeshi letu ndilo litakalo shinda.
174. Basi waachilie mbali kwa muda.
175. Na watazame, nao wataona.
176. Je! Wanaihimiza adhabu yetu?
177. Basi itakapo shuka uwanjani kwao, itakuwa asubuhi
mbaya kwa walio onywa.
178. Na waache kwa muda.
179. Na tazama, na wao wataona.
180. Subhana Rabbi'l'Izzat Ametakasika Mola Mlezi Mwenye
enzi na yale wanayo mzulia.
181. Na Salamu juu ya Mitume.
182. Na sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu Mola Mlezi wa
walimwengu wote.
|