1 - 50
1. Naapa kwa nyota inapo tua,
2. Mwenzenu huyu hakupotea, wala hakukosea.
3. Wala hatamki kwa matamanio.
4. Hayakuwa haya ila ni ufunuo ulio funuliwa;
5. Amemfundisha aliye mwingi wa nguvu,
6. Mwenye kutua, akatulia,
7. Naye yuko juu kabisa upeo wa macho.
8. Kisha akakaribia na akateremka.
9. Akawa ni kama baina ya mipinde miwili, au karibu zaidi.
10. Akamfunulia mja wake (Mwenyezi Mungu) alicho mfunulia.
11. Moyo haukusema uwongo uliyo yaona.
12. Je! Mnabishana naye kwa aliyo yaona?
13. Na akamwona mara nyingine,
14. Penye Mkunazi wa mwisho.
15. Karibu yake ndiyo ipo Bustani inayo kaliwa.
16. Kilipo ufunika huo Mkunazi hicho kilicho ufunuika.
17. Jicho halikuhangaika wala halikuruka mpaka.
18. Kwa yakini aliona katika Ishara kubwa kabisa za Mola
wake Mlezi.
19. Je! Mmemuona Lata na Uzza?
20. Na Manaat, mwingine wa tatu?
21. Je! Nyinyi mnao wana wanaume na Yeye ndio awe na
wanawake?
22. Huo ni mgawanyo wa dhulma!
23. Hayo hayakuwa ila ni majina mliyo wapa nyinyi na baba
zenu. Mwenyezi Mungu hakuleta uthibitisho wowote juu ya hayo. Hawafuati ila
dhana tu na kipendacho nafsi. Na kwa yakini uwongofu ulikwisha wafikia kutoka
kwa Mola wao Mlezi.
24. Ati mtu anakipata kila anacho kitamani?
25. Mwenyezi Mungu tu ndiye Mwenye dunia na Akhera.
26. Na wako Malaika wangapi mbinguni, ambao uombezi wao hautafaa
chochote isipo kuwa baada ya Mwenyezi Mungu kutoa idhini kwa amtakaye na
kumridhia.
27. Hakika wasio amini Akhera bila ya shaka wao ndio
wanawaita Malaika kwa majina ya kike.
28. Nao hawana ujuzi wowote kwa hayo isipo kuwa wanafuata
dhana tu. Na dhana haisaidii chochote mbele ya haki.
29. Basi mwachilie mbali anaye upa kisogo ukumbusho wetu,
na wala hataki ila maisha ya dunia.
30. Huo ndio mwisho wao wa ujuzi. Hakika Mola wako Mlezi
ndiye anaye mjua zaidi mwenye kuipotea njia yake, na Yeye ndiye anaye mjua
zaidi mwenye kuongoka.
31. Ni vya Mwenyezi Mungu vyote viliomo mbinguni na viliomo
katika ardhi, ili awalipe walio tenda ubaya kwa waliyo yatenda, na walio tenda
mema awalipe mema.
32. Ambao wanajiepusha na madhambi makuu na vitendo
vichafu, isipo kuwa makosa khafifu. Hakika Mola wako Mlezi ni Mkunjufu wa
maghfira, naye anakujueni sana tangu alipo kuumbeni kutoka kwenye ardhi, na
mlipo kuwa mimba matumboni mwa mama zenu. Basi msijisifu usafi. Yeye anamjua
sana mwenye kujikinga na maovu.
33. Je! Umemwona yule aliye geuka?
34. Na akatoa kidogo, kisha akajizuia?
35. Je! Anayo huyo ilimu ya ghaibu, basi ndio anaona?
36. Au hakuambiwa yaliyomo katika Vitabu vya Musa?
37. Na vya Ibrahimu aliye timiza ahadi?
38. Ya kwamba hakika nafsi iliyo beba madhambi haibebi
madhambi ya mwengine?
39. Na ya kwamba hatapata mtu ila aliyo yafanya mwenyewe?
40. Na kwamba vitendo vyake vitaonekana?
41. Kisha ndio atalipwa malipo yake kwa ukamilifu.
42. Na kwamba kwao Mola wako Mlezi ndio mwisho.
43. Na kwamba Yeye ndiye anaye leta kicheko na kilio.
44. Na kwamba Yeye ndiye anaye fisha na kuhuisha.
45. Na kwamba Yeye ndiye aliye umba jozi, dume na jike
46. Kutokana na mbegu ya uzazi inapo miminwa.
47. Na kwamba ni juu yake ufufuo mwengine.
48. Na kwamba ni Yeye ndiye anaye tosheleza na kukinaisha.
49. Na kwamba hakika Yeye ndiye Mola Mlezi wa nyota ya
Shii'ra.
50. Na kwamba Yeye ndiye aliye waangamiza A'di wa kwanza,
|