51 - 78
51. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo
ikanusha?
52. Humo katika kila matunda zimo namna mbili.
53. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo
ikanusha?
54. Wawe wameegemea matandiko yenye bit'ana ya hariri
nzito; na matunda ya Bustani hizo yapo karibu.
55. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo
ikanusha?
56. Humo watakuwamo wanawake watulizao macho yao;
hajawagusa mtu kabla yao wala jini.
57. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo
ikanusha?
58. Kama kwamba wao ni yakuti na marijani.
59. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo
ikanusha.
60. Ati yaweza kuwa malipo ya ihsani ila ihsani?
61. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo
ikanusha?
62. Na zaidi ya hizo zipo Bustani nyengine mbili.
63. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo
ikanusha?
64. Za kijani kibivu.
65. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo ikanusha?
66. Na chemchem mbili zinazo furika.
67. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo
ikanusha?
68. Imo humo miti ya matunda, na mitende na mikomamanga.
69. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo
ikanusha?
70. Humo wamo wanawake wema wazuri.
71. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo
ikanusha?
72. Wanawake wazuri wanao tawishwa katika makhema.
73. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo
ikanusha?
74. Hajawagusa mtu wala jini kabla yao.
75. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo
ikanusha?
76. Wameegemea juu ya matakia ya kijani na mazulia mazuri.
77. Basi ni ipi katika neema za Mola wenu Mlezi mnayo
ikanusha?
78. Limetukuka jina la Mola wako Mlezi Mwenye utukufu na
ukarimu.
|