74. SURAT AL-MUDDATHTHIR
(Imeteremka
Makka)
Sura hii tukufu inamhimiza
Mtume wa Mwenyezi Mungu s.a.w. awaonye watu wake, na amtukuze Mwenyezi Mungu
Mtukufu, na ayaache yasiyo faa kutokana naye, na imesimulia khabari za
kupulizwa barugumu na shida za adhabu zitazo washukia makafiri. Na inamuamrisha
Mtume s.a.w. amwachilie mbali anaye pinga fadhila alizo fanyiwa na kisha
anatumai bado azidishiwe bila ya kutambua wala shukrani. Na Sura imebainisha
vipi kulikuwa kufikiri kwa huyo mwenye kupinga na kuikataa Qur'ani, na
ikafafanua vipi itakuwa adhabu yake katika Moto wa Saqar ambao unaelezwa kwa
njia ya kutisha na kukhofisha. Na ikataja khabari za nafsi kwa zinavyo chuma
kheri au shari, na ikaeleza hali ya watu wa mkono wa kulia na wanavyo wakejeli
wakosefu kwa kuwauliza nini kilicho wasukumiza Motoni. Na Sura imekhitimisha
kwa kusimulia kuwa Qur'ani ni ya mwenye kutaka kuwaidhika, na wenye kuwaidhika
ndio watu wachamngu na ndio wenye kupata msamaha.
KWA JINA LA MWENYEZI
MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU
1. Ewe uliye jigubika!
2. Simama uonye!
3. Na Mola wako Mlezi mtukuze!
4. Na nguo zako, zisafishe.
5. Na yaliyo machafu yahame!
6. Wala usitoe kwa kutaraji kuzidishiwa.
7. Na kwa ajili ya Mola wako Mlezi, subiri!
8. Basi litapo pulizwa barugumu,
9. Siku hiyo, basi, itakuwa siku ngumu.
10. Kwa makafiri haitakuwa nyepesi.
11. Niache peke yangu na niliye muumba;
12. Na nikamjaalia awe na mali mengi,
13. Na
wana wanao onekana,
14. Na
nikamtgenezea mambo vizuri kabisa.
15. Kisha anatumai nimzidishie!
16. Hasha!
Kwani hakika yeye alikuwa akizifanyia inadi Aya zetu!
17. Nitamtesa kwa mateso yasio wezekana.
18. Kwani hakika yeye alifikiri na akapima.
19. Basi ameangamia! Vipi alivyo pima!
20. Tena ameangamia! Vipi alivyo pima!
21. Kisha akatazama,
22. Kisha akakunja kipaji, na akanuna.
23. Kisha akaipa kisogo haki, na akatakabari.
24. Na akasema: Haya si chochote ila ni uchawi ulio
nukuliwa.
25. Haya si chochote ila kauli ya binaadamu.
26.
Nitakuja mtia kwenye Moto wa Saqar.
27. Na
nini kitakujuulisha ni nini huo Moto wa Saqar?
28. Haubakishi wala hausazi.
29. Unababua ngozi iwe nyeusi.
30. Juu yake wapo kumi na tisa.
31. Na hatukuwafanya walinzi wa Motoni ila ni Malaika, wala
hatukuifanya idadi yao hiyo ila kuwatatanisha walio kufuru, wapate kuwa na
yakini walio pewa Kitabu, na wazidi Imani wale walio amini, wala wasiwe na
shaka walio pewa Kitabu na Waumini, na wapate kusema wenye maradhi katika nyoyo
zao na makafiri: Mwenyezi Mungu amekusudia nini kwa mfano huu? Ndio kama hivyo
Mwenyezi Mungu humwacha apotee amtakaye, na humwongoa amtakaye. Na hapana
yeyote anaye jua majeshi ya Mola wako Mlezi ila Yeye tu. Na haya si chochote
ila ni ukumbusho kwa binaadamu.
32. Hasha!
Naapa kwa mwezi!
33. Na kwa usiku unapo kucha!
34. Na kwa asubuhi inapo pambazuka!
35. Hakika huo Moto ni katika mambo yaliyo makubwa kabisa!
36. Ni onyo kwa binaadamu,
37. Kwa anaye taka miongoni mwenu kutangulia au kuchelewa.
38. Kila nafsi imo rahanini kwa mabaya iliyo yachuma.
39. Isipo kuwa watu wa kuliani.
40. Hao watakuwa katika Mabustani, wawe wanaulizana
41. Khabari za wakosefu:
42. Ni nini kilicho kupelekeni Motoni?
43. Waseme: Hatukuwa miongoni walio kuwa wakisali.
44. Wala hatukuwa tukiwalisha masikini.
45. Na tulikuwa tukizama pamoja na walio zama katika maovu.
46. Na tulikuwa tukiikanusha siku ya malipo.
47. Mpaka yakini ilipo tufikia.
48. Basi hautawafaa kitu uombezi wa waombezi.
49. Basi wana nini hata wanapuuza onyo hili?
50. Kama kwamba wao ni mapunda walio timuliwa,
|