85. SURAT AL-BURUUJ
(Imeteremka
Makka)
Sura hii ni ya maliwaza na kuwapa
mawaidha Waumini, na kuwatisha na kuwaonya wenye inadi. Imeanzia kwa kiapo
chake Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa madhaahiri yanayo onekana ya uweza wake ya
kwamba wapinzani wanao waudhi Waumini watafukuzwa kwenye uwanja wa rehema, kama
walivyo fukuzwa walio kwenda mwendo wao katika mataifa yaliyo tangulia. Na Sura
ikaingia kusimulia kisa cha hao majabari walivyo watendea Waumini, na
ikafuatiza kwa kuwapa ahadi Waumini na kuwakhofisha majeuri, na kwamba Haki
katika kila zama hupingwa na wapinzani. Na kwamba Qur'ani, ambayo ndiyo mwega
wa Haki, na wangaikadhibisha watu fulani, lakini hiyo iko mbali kabisa na
shaka, kwa sababu hakika hiyo iko katika Lauh'un Mahfuudh, Ubao Ulio Hifadhiwa
ulioko kwa Mwenyezi Mungu.
KWA JINA LA MWENYEZI
MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU
1. Naapa kwa mbingu yenye Buruji!
2. Na kwa siku iliyo ahidiwa!
3. Na kwa shahidi na kinacho shuhudiwa!
4. Wameangamizwa watu wa makhandaki
5. Yenye
moto wenye kuni nyingi,
6. Walipo
kuwa wamekaa hapo,
7. Na wao
ni mashahidi wa yale waliyo kuwa wakiwafanyia Waumini.
8. Nao
hawakuona baya lolote kwao ila kuwa wakimuamini Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu,
Msifiwa,
9. Ambaye
anao ufalme wa mbingu na ardhi; na Mwenyezi Mungu ni shaahidi wa kila kitu.
10. Hakika
walio wafitini Waumini wanaume na Waumini wanawake, kisha hawakutubu, basi
watapata adhabu ya Jahannamu na watapata adhabu ya kuungua.
11. Hakika
walio amini na wakatenda mema watapata Bustani zenye mito ipitayo kati yake. Huko ndiko kufuzu kukubwa.
12. Hakika
kutesa kwa Mola wako Mlezi ni kukali.
13. Yeye ndiye
anaye anzisha na ndiye anaye rejeza tena,
14. Naye ni
Mwenye kusamehe, Mwenye mapenzi,
15. Mwenye Kiti
cha Enzi, Mtukufu,
16.
Atendaye ayatakayo.
17. Je!
Zimekuwasilia khabari za majeshi?
18. Ya
Firauni na Thamudi?
19. Lakini
walio kufuru wamo katika kukadhibisha.
20. Na
Mwenyezi Mungu nyuma yao amewazunguka.
21. Bali hii ni
22. Katika Ubao Ulio Hifadhiwa.
|