Table of Contents | Words: Alphabetical - Frequency - Inverse - Length - Statistics | Help | IntraText Library

Qu'rani

IntraText CT - Text

  • 95. SURAT AT-TIN
Previous - Next

Click here to show the links to concordance

95. SURAT AT-TIN

(Imeteremka Makka)

Mwenyezi Mungu anaapa katika Sura hii kwa matunda mawili yenye baraka, na pahala pawili pazuri, ya kwamba Yeye hakika amemuumba mtu kwa njia kunjufu kabisa, kwa kumkamilishia akili, na uwezo wa kutaka na kutotaka, na mengineyo katika sifa za ukamilifu. Kisha Aya zikataja kuwa mtu hakusimama kwa mujibu wa alivyo umbiwa, bali akateremka kwa daraja mpaka akawa wa chini kabisa, isipo kuwa walio amini na wakatenda mema kati yao. Hao Mwenyezi Mungu amewakunjulia vipawa. Kisha Sura imewageukia kuwakemea wanao kadhibisha kufufuliwa baada ya kudhihiri dalili zote za uweza wa Mwenyezi Mungu na khabari za hikima yake.

KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

1. Naapa kwa tini na zaituni!

2. Na kwa Mlima wa Sinai!

3. Na kwa mji huu wenye amani!

4. Bila ya shaka tumemuumba mtu kwa umbo lilio bora kabisa.

5. Kisha tukamrudisha kuwa chini kuliko walio chini!

6. Lakini wale walio amini na wakatenda mema, hao watapata ujira usio kwisha.

7. Basi ni kipi baadaye kitacho kukukadhibishia malipo?

8. Kwani Mwenyezi Mungu si muadilifu kuliko mahakimu wote?

 




Previous - Next

Table of Contents | Words: Alphabetical - Frequency - Inverse - Length - Statistics | Help | IntraText Library

Best viewed with any browser at 800x600 or 768x1024 on Tablet PC
IntraText® (V89) - Some rights reserved by EuloTech SRL - 1996-2007. Content in this page is licensed under a Creative Commons License