100. SURAT AL-A'ADIYAAT
(Imeteremka
Makka)
Mwenyezi Mungu Mtukufu
ameapa katika kifungulio cha Sura hii kwa farasi wa Jihadi, kwamba hakika
mwanaadamu bila ya shaka ni mwingi wa kuikufuru neema ya Mola wake Mlezi. Na
kwamba juu ya hivyo katika Akhera bila ya shaka atakuwa ni shahidi dhidi ya
nafsi yake kwa aliyo kuwa nayo. Na kwamba bila ya shaka yeye kwa kuyapenda mali
ni bakhili na mwenye choyo juu yake. Na khatimaye ametaja khabari za
kufufuliwa, na akazindua kuwa ipo hisabu na malipo.
KWA JINA LA MWENYEZI
MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU
1. Naapa kwa farasi wendao mbio wakipumua,
2. Na wakitoa moto kwa kupiga kwato zao chini,
3.
Wakishambulia wakati wa asubuhi,
4. Huku
wakitimua vumbi,
5. Na wakijitoma
kati ya kundi,
6. Hakika
mwanaadamu ni mtovu wa fadhila kwa Mola wake Mlezi!
7. Na hakika
yeye mwenyewe bila ya shaka ni shahidi wa hayo!
8. Naye hakika
bila ya shaka ana nguvu za kupenda mali!
9. Kwani hajui
watakapo fufuliwa waliomo makaburini?
10. Na
yakakusanywa yaliomo vifuani?
11. Kuwa hakika
Mola wao Mlezi siku hiyo bila ya shaka atakuwa na khabari zao wote!
|