Table of Contents | Words: Alphabetical - Frequency - Inverse - Length - Statistics | Help | IntraText Library

Qu'rani

IntraText CT - Text

  • 114. SURAT ANNAS
Previous - Next

Click here to show the links to concordance

114. SURAT ANNAS

(Imeteremka Makka)

Katika Sura hii Mwenyezi Mungu anamuamrisha Nabii wake s.a.w. amwendee Yeye amwombe ulinzi kumkinga na shari kubwa zinazo washinda watu wengi kuzitambua kwa sababu zinatokana na matamanio yao, na pumbao lao, basi wakatumbukia katika yale yale wanayo katazwa.
Hiyo ndiyo shari ya wasiwasi wa Shetani, anaye jificha machoni, au hujidhihirisha kwa kificho; wasiwasi wake ni kwa hila na khadaa.

KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

1. Sema: Ninajikinga kwa Mola Mlezi wa wanaadamu,

2. Mfalme wa wanaadamu,

3. Mungu wa wanaadamu,

4. Na shari ya wasiwasi wa Shetani, Khannas,

5. Anaye tia wasiwasi katika vifua vya watu,

6. Kutokana na majini na wanaadamu.

 




Previous - Next

Table of Contents | Words: Alphabetical - Frequency - Inverse - Length - Statistics | Help | IntraText Library

Best viewed with any browser at 800x600 or 768x1024 on Tablet PC
IntraText® (V89) - Some rights reserved by EuloTech SRL - 1996-2007. Content in this page is licensed under a Creative Commons License