Chapter 9
1 Yesu
akaendelea kuwaambia, "Kweli nawaambieni, wako wengine papa hapa ambao hawatakufa
kabla ya kuuona Ufalme wa Mungu ukija kwa enzi."
2 Baada ya
siku sita, Yesu aliwachukua Petro, Yakobo na Yohane juu ya mlima mrefu peke
yao. Huko, Yesu akageuka sura mbele yao,
3 mavazi
yake yakang`aa, yakawa meupe sana, jinsi dobi yeyote duniani asingeweza
kuyafanya meupe.
4 Eliya na
Mose wakawatokea, wakazungumza na Yesu.
5 Petro
akamwambia Yesu, "Mwalimu, ni vizuri sana kwamba tuko hapa. Basi, afadhali
tujenge vibanda vitatu: kimoja chako, kimoja cha Mose na kimoja cha
Eliya."
6 Yeye na
wenzake waliogopa hata hakujua la kusema.
7 Kisha
likatokea wingu likawafunika, na sauti ikasikika kutoka katika hilo wingu,
"Huyu ni Mwanangu mpendwa, msikilizeni."
8 Mara
wanafunzi hao wakatazama tena, lakini hawakumwona mtu mwingine, ila Yesu peke
yake pamoja nao.
9
Walipokuwa wakishuka mlimani, Yesu aliwakataza wasimwambie mtu yeyote mambo
waliyoyaona, mpaka Mwana wa Mtu atakapokuwa amefufuka kutoka wafu.
10 Basi,
wakashika agizo hilo, lakini wakawa wanajadiliana wao kwa wao maana ya kufufuka
kutoka wafu.
11
Wakamwuliza Yesu, "Mbona walimu wa Sheria wanasema kwamba ni lazima Eliya
aje kwanza?"
12 Naye
akawajibu, "Naam, Eliya anakuja kwanza kutayarisha yote. Hata hivyo, kwa
nini basi imeandikwa katika Maandiko Matakatifu kwamba Mwana wa Mtu atapatwa na
mateso mengi na kudharauliwa?
13 Lakini
nawaambieni, Eliya amekwisha kuja, nao wakamtendea walivyotaka kama
ilivyoandikwa juu yake."
14
Walipowafikia wale wanafunzi wengine, waliona umati mkubwa wa watu hapo. Na
baadhi ya walimu wa Sheria walikuwa wanajadiliana nao.
15 Mara tu
ule umati wa watu ulipomwona, wote walishangaa sana, wakamkimbilia wamsalimu.
16 Yesu
akawauliza, "Mnajadiliana nini nao?"
17 Hapo
mtu mmoja katika ule umati wa watu akamjibu, "Mwalimu, nimemleta mwanangu
kwako, ana pepo aliyemfanya kuwa bubu.
18 Kila
mara anapomvamia, humwangusha chini na kumfanya atokwe na povu kinywani,
akisaga meno na kuwa mkavu mwili wote. Niliwaomba wanafunzi wako wamtoe huyo
pepo lakini hawakuweza."
19 Yesu
akawaambia, "Enyi kizazi kisicho na imani! Nitakaa nanyi mpaka lini?
Nitawavumilia mpaka lini? Mleteni kwangu."
20
Wakampeleka. Mara tu huyo pepo alipomwona Yesu, alimtia mtoto kifafa, naye
mtoto akaanguka chini, akagaagaa na kutoka povu kinywani. Yesu akamwuliza baba
yake huyo mtoto,
21
"Amepatwa na mambo hayo tangu lini?" Naye akamjibu, "Tangu utoto
wake.
22 Na mara
nyingi pepo huyo amemwangusha motoni na majini, ili amwangamize kabisa. Basi,
ikiwa waweza, utuhurumie na kutusaidia!"
23 Yesu
akamwambia, "Eti ikiwa waweza! Mambo yote yanawezekana kwa mtu aliye na
imani."
24 Hapo,
huyo baba akalia kwa sauti, "Naamini! Lakini imani yangu haitoshi,
nisaidie!"
25 Yesu
alipouona umati wa watu unaongezeka upesi mbele yake, alimkemea yule pepo
mchafu, "Pepo unayemfanya huyu mtoto kuwa bubu-kiziwi, nakuamuru, mtoke
mtoto huyu wala usimwingie tena!"
26 Hapo
huyo pepo alipaaza sauti, akamwangusha huyo mtoto chini, kisha akamtoka. Mtoto
alionekana kama maiti, hata wengine walisema, "Amekufa!"
27 Lakini
Yesu akamshika mkono, akamwinua, naye akasimama.
28 Yesu
alipoingia nyumbani, wanafunzi wake walimwuliza kwa faragha, "Kwa nini sisi
hatukuweza kumtoa?"
29 Naye
akawaambia, "Pepo wa aina hii hawezi kutoka isipokuwa kwa sala tu."
30 Yesu na
wanafunzi wake waliondoka hapo, wakaendelea na safari kupitia wilaya ya
Galilaya. Yesu hakupenda watu wajue alipokuwa,
31 kwa
sababu alikuwa anawafundisha wanafunzi wake. Aliwaambia, "Mwana wa Mtu
atakabidhiwa kwa watu ambao watamuua; lakini siku ya tatu baada ya kuuawa
atafufuka."
32
Wanafunzi hawakufahamu jambo hilo. Wakaogopa kumwuliza.
33 Basi,
walifika Kafarnaumu. Na alipokuwa nyumbani, aliwauliza, "Mlikuwa
mnajadiliana nini njiani?"
34 Lakini
wao wakanyamaza, maana njiani walikuwa wamebishana ni nani aliye mkuu kati yao.
35 Yesu
akaketi chini, akawaita wale kumi na wawili, akawaambia, "Yeyote anayetaka
kuwa wa kwanza lazima awe wa mwisho na kuwa mtumishi wa wote."
36 Kisha
akamchukua mtoto mdogo, akamsimamisha kati yao, akamku mbatia, halafu
akawaambia,
37
"Anayempokea mtoto kama huyu kwa jina langu, ananipokea mimi; na
anayenipokea mimi, hanipokei mimi tu, bali anampokea yule aliyenituma."
38 Yohane
akamwambia, "Mwalimu, tumemwona mtu mmoja akitoa pepo kwa kulitumia jina
lako, nasi tukajaribu kumkataza kwa kuwa yeye si mmoja wetu."
39 Lakini
Yesu akasema, "Msimkataze, maana hakuna mtu anayefanya muujiza kwa jina
langu, na papo hapo akaweza kusema mabaya juu yangu.
40 Maana,
asiyepingana nasi, yuko upande wetu.
41 Mtu
yeyote atakeyewapeni kikombe cha maji ya kunywa kwa sababu ninyi ni watu wake
Kristo, hakika hatakosa kupata tuzo lake.
42
"Mtu yeyote atakayemfanya mmoja wa hawa wadogo wanaoniamini atende dhambi,
ingekuwa afadhali kwa mtu huyo kufungiwa shingoni mwake jiwe kubwa la kusagia
na kutupwa baharini.
43 Mkono
wako ukikukosesha, ukate! Afadhali kuingia kwenye uzima bila mkono mmoja,
kuliko kuwa na mikono miwili na kwenda katika moto wa Jehanamu.*fe*
44 missing
45 Na mguu
wako ukikukosesha, ukate! Afadhali kuingia katika uzima bila mguu mmoja, kuliko
kuwa na miguu yote miwili na kutupwa katika moto wa Jehanamu.*ff*
46 missing
47 Na
jicho lako likikukosesha, ling`oe! Afadhali kuingia katika utawala wa Mungu
ukiwa na jicho moja tu, kuliko kuwa na macho yako yote mawili na kutupwa katika
moto wa Jehanamu.
48 Humo
wadudu wake hawafi, na moto hauzimiki. ic\is Mawe ya kusagia (Marko 9:42)\ie
moto hauzimiki. moto hauzimiki.
49
"Maana kila mmoja atakolezwa kwa moto.
50 Chumvi
ni nzuri, lakini ikipoteza ladha yake, itakolezwa na nini? Muwe na chumvi ndani
yenu na kudumisha amani kati yenu."
|