Chapter 11
1
Walipokuwa wanakaribia Yerusalemu walifika Bethfage na Bethania, karibu na
mlima wa Mizeituni. Hapo aliwatuma wawili wa wanafunzi wake,
2
akawaambia, "Nendeni katika kijiji kilicho mbele yenu. Mtakapokuwa
mnaingia humo, mtakuta mwana punda amefungwa ambaye bado hajatumiwa na mtu.
Mfungueni mkamlete.
3 Kama mtu
akiwauliza, `Mbona mnafanya hivyo?` Mwambieni, `Bwana anamhitaji na atamrudisha
hapa mara."` ic\is Bethania (Marko 11:1)\ie
4 Basi,
wakaenda, wakamkuta mwana punda barabarani amefungwa mlangoni. Walipokuwa
wakimfungua,
5 baadhi
ya watu waliokuwa wamesimama hapo wakawauliza "Kwa nini mnamfungua huyo mwana
punda?"
6
Wanafunzi wakajibu kama Yesu alivyokuwa amewaambia; nao wakawaacha waende zao.
7
Wakampelekea Yesu huyo mwana punda. Wakatandika mavazi yao juu ya huyo mwana
punda, na Yesu akaketi juu yake.
8 Watu
wengi wakatandaza mavazi yao barabarani; wengine wakatandaza matawi ya miti
waliyoyakata mashambani.
9 Watu
wote waliotangulia na wale waliofuata wakapaaza sauti zao wakisema,
"Hosana! Abarikiwe huyo ajaye kwa jina la Bwana!
10
Ubarikiwe Ufalme ujao wa baba yetu Daudi. Hosana juu mbinguni!"
11 Yesu
aliingia mjini Yerusalemu akaenda moja kwa moja mpaka Hekaluni, akatazama kila
kitu kwa makini. Lakini kwa vile ilikwisha kuwa jioni, akaenda Bethania pamoja
na wale kumi na wawili.
12 Kesho
yake, walipokuwa wanatoka Bethania, Yesu aliona njaa.
13 Basi,
akaona kwa mbali mtini wenye majani mengi. Akauendea ili aone kama ulikuwa na
tunda lolote. Alipoufikia, aliukuta bila tunda lolote ila majani matupu, kwa
vile hayakuwa majira ya mtini kuzaa matunda.
14 Hapo
akauambia mtini, "Tangu leo hata milele mtu yeyote asile matunda
kwako." Nao wanafunzi wake walisikia maneno hayo.
15 Basi,
wakafika Yerusalemu. Yesu akaingia Hekaluni, akaanza kuwafukuza nje watu
waliokuwa wanauza na kununua vitu humo ndani. Akazipindua meza za wale
waliokuwa wakibadilishana fedha na viti vya wale waliokuwa wakiuza njiwa.
16
Hakumruhusu mtu yeyote kupitia Hekaluni akichukua kitu.
17 Kisha
akawafundisha, "Imeandikwa: `Nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala kwa ajili
ya mataifa yote!` Lakini ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyang`anyi!"
18
Makuhani wakuu na walimu wa Sheria waliposikia hayo, walianza kutafuta njia ya
kumwangamiza. Lakini walimwogopa kwa sababu umati wa watu ulishangazwa na
mafundisho yake.
19
Ilipokuwa jioni, Yesu na wanafunzi wake waliondoka mjini.
20 Asubuhi
na mapema, walipokuwa wanapita, waliuona ule mtini umenyauka wote, hata mizizi.
21 Petro
aliukumbuka, akamwambia Yesu, "Mwalimu, tazama! Ule mtini ulioulaani,
umenyauka!"
22 Yesu
akawaambia, "Mwaminini Mungu.
23
Nawaambieni kweli, mtu akiuambia mlima huu: `Ng`oka ukajitose baharini` bila
kuona shaka moyoni mwake, ila akaamini kwamba mambo yote anayosema yanafanyika,
atafanyiwa jambo hilo.
24 Kwa
hiyo nawaambieni, mnaposali na kuomba kitu, aminini kwamba mmekipokea, nanyi
mtapewa.
25
Mnaposimama kusali, sameheni kila mtu aliyewakosea chochote, ili Baba yenu
aliye mbinguni awasamehe ninyi makosa yenu.*fg* hata Baba yenu aliye mbinguni
hatawasamehe ninyi makosa yenu."
26 missing
27 Basi,
wakafika tena Yerusalemu. Yesu alipokuwa akitembea Hekaluni, makuhani wakuu,
walimu wa Sheria na wazee walimwendea,
28
wakamwuliza, "Unafanya mambo haya kwa mamlaka gani? Nani aliyekupa mamlaka
ya kufanya mambo haya?"
29 Lakini
Yesu akawaambia, "Nitawaulizeni swali moja; mkinijibu, na pia
nitawaambieni ni kwa mamlaka gani ninafanya mambo haya.
30 Je,
mamlaka ya Yohane ya kubatiza yalitoka mbinguni ama kwa watu? Nijibuni."
31
Wakaanza kujadiliana, "Tukisema, `Yalitoka mbinguni`, atatuuliza, `Basi,
mbona hamkumsadiki?`
32 Na
tukisema, `Yalitoka kwa watu..."` (Waliogopa umati wa watu maana wote
waliamini kwamba Yohane alikuwa kweli nabii.)
33 Basi,
wakamjibu Yesu, "Sisi hatujui." Naye Yesu akawaambia, "Nami pia
sitawaambieni ninafanya mambo haya kwa mamlaka gani."
|