Chapter 12
1 Yesu
alianza kusema nao kwa mifano: "Mtu mmoja alilima shamba la mizabibu.
Akalizungushia ukuta, na katikati yake akachimba kisima cha kusindikia divai,
akajenga mnara pia. Akalikodisha shamba hilo kwa wakulima, akasafiri hadi nchi
ya mbali.
2 Wakati
wa mavuno, alimtuma mtumishi wake kwa wale wakulima akamletee sehemu ya mazao
ya shamba lake.
3 Wale
wakulima wakamkamata, wakampiga, wakamrudisha mikono mitupu.
4 Akatuma
tena mtumishi mwingine; huyu wakamuumiza kichwa na kumtendea vibaya.
5 Mwenye
shamba akatuma mtumishi mwingine tena, na huyo wakamuua. Wengine wengi
waliotumwa, baadhi yao walipigwa, na wengi wakauawa.
6
Alibakiwa bado na mtu mmoja, yaani mwanawe mpendwa. Mwishowe akamtuma huyo akisema,
`Watamheshimu mwanangu.`
7 Lakini
hao wakulima wakaambiana, `Huyu ndiye mrithi, basi, tumuue ili urithi wake uwe
wetu!`
8 Kwa hiyo
wakamkamata, wakamuua na kumtupa nje ya lile shamba la mizabibu. ic Mnara ndani
ya shamba la mizabibu (Marko 12:1)
9
"Basi, mwenye shamba atafanya nini? Atakuja kuwaangamiza hao wakulima na
kulikodisha hilo shamba la mizabibu kwa watu wengine.
10 Je,
hamjasoma Maandiko haya? `Jiwe walilokataa waashi sasa limekuwa jiwe kuu la
msingi.
11 Bwana
ndiye aliyefanya jambo hili, nalo ni la ajabu sana kwetu."`
12
Makuhani wakuu, walimu wa Sheria na wazee walifahamu ya kwamba mfano huo
ulikuwa unawahusu. Kwa hiyo walijaribu kumtia nguvuni, lakini waliogopa umati
wa watu. Basi, wakamwacha wakaenda zao.
13 Basi,
baadhi ya Mafarisayo na wafuasi wa kikundi cha Herode walitumwa ili wamtege
Yesu kwa maneno yake.
14
Wakamwendea, wakamwambia, "Mwalimu, tunajua kwamba wewe ni mtu mwaminifu
unayesema ukweli mtupu, wala humjali mtu yeyote. Wala cheo cha mtu si kitu
kwako, lakini wafundisha ukweli kuhusu njia ya Mungu. Je, ni halali kulipa kodi kwa Kaisari, au la?
Tulipe au tusilipe?"
15 Lakini Yesu
alijua unafiki wao, akawaambia, "Mbona mnanijaribu? Nionyesheni
sarafu."
16
Wakamwonyesha. Naye akawauliza, "Sura na chapa hii ni ya nani?"
Wakamjibu, "Ni ya Kaisari."
17 Basi, Yesu
akawaambia, "Mpeni Kaisari yaliyo yake Kaisari na Mungu yaliyo yake
Mungu." Wakashangazwa sana naye.
18 Masadukayo
wasemao kwamba hakuna ufufuo walimwendea Yesu, wakamwuliza,
19
"Mwalimu, Mose alituagiza hivi: `Mtu akifa na kuacha mke bila mtoto, ndugu
yake lazima amchukue huyo mama mjane amzalie watoto ndugu yake marehemu.`
20 Basi,
kulikuwa na ndugu saba. Wa kwanza alioa, akafa bila kuacha mtoto.
21 Ndugu
wa pili akamwoa huyo mjane, naye pia akafa bila kuacha mtoto; na ndugu watatu
hali kadhalika.
22 Wote
saba walikufa bila kuacha mtoto. Mwishowe yule mama mjane naye akafa.
23 Basi,
siku watu watakapofufuka, mama huyo atakuwa mke wa nani? Maana wote saba
walikuwa wamemwoa."
24 Yesu
akawaambia, "Ninyi mmekosea sana, kwa sababu hamjui Maandiko Matakatifu
wala nguvu ya Mungu.
25 Maana
wafu watakapofufuka, hawataoa wala kuolewa; watakuwa kama malaika wa mbinguni.
26 Lakini
kuhusu kufufuliwa kwa wafu, je, hamjasoma kitabu cha Mose katika sehemu
inayohusu kile kichaka kilichokuwa kinawaka moto? Mungu alimwambia Mose, `Mimi
ni Mungu wa Abrahamu, Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo.`
27 Basi, yeye si Mungu wa wafu, bali ni Mungu wa walio hai.
Ninyi mmekosea sana!"
28 Mmojawapo wa walimu wa Sheria alifika, akasikia
mabishano yao. Alipoona kwamba Yesu aliwajibu vyema, akajitokeza akamwuliza,
"Katika amri zote ni ipi iliyo ya kwanza?"
29 Yesu akamjibu, "Ya kwanza ndiyo hii: `Sikiliza,
Israeli! Bwana Mungu wetu ndiye peke yake Bwana.
30 Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa roho
yako yote, kwa akili yako yote na kwa nguvu zako zote.`
31 Na ya pili ndiyo hii: `Mpende jirani yako kama
unavyojipenda mwenyewe.` Hakuna amri nyingine iliyo kuu kuliko hizi."
32 Basi, yule mwalimu wa Sheria akamwambia, "Vyema
Mwalimu! Umesema kweli kwamba Mungu ni mmoja tu wala hakuna mwingine ila yeye.
33 Na ni lazima mtu kumpenda Mungu kwa moyo wote, kwa akili
yote, na kwa nguvu zote, na kumpenda jirani yake kama anavyojipenda mwenyewe.
Jambo hili ni muhimu zaidi kuliko dhabihu na sadaka zote za kuteketezwa."
34 Yesu alipoona kwamba huyu mtu alimjibu kwa ujasiri,
akamwambia, "Wewe huko mbali na Ufalme wa Mungu." Baada ya hayo,
hakuna mtu aliyethubutu tena kumwuliza kitu.
35 Wakati Yesu alipokuwa akifundisha Hekaluni, aliuliza,
"Mbona walimu wa Sheria wanasema ya kwamba Kristo ni mwana wa Daudi?
36 Daudi mwenyewe akiongozwa na Roho Mtakatifu alisema:
`Bwana alimwambia Bwana wangu: Keti upande wangu wa kulia, Mpaka nitakapowaweka
adui zako chini ya miguu yako."`
37 "Daudi mwenyewe anamwita Kristo Bwana. Basi, Kristo
atakuwaje mwanae?" Umati wa watu ulikuwa ukimsikiliza kwa furaha.
38 Katika mafundisho yake, Yesu alisema, "Jihadharini
na walimu wa Sheria ambao hupenda kupitapita wamejivalia kanzu ndefu na
kusalimiwa na watu kwa heshima sokoni; hupenda kuketi mahali pa heshima katika
masunagogi,
39 na kuchukua nafasi za heshima katika karamu.
40 Huwanyonya wajane huku wakijisingizia kusali sala ndefu.
Siku ya hukumu watapata adhabu kali!"
41 Yesu alikuwa ameketi karibu na sanduku la hazina. Akawa
anatazama jinsi watu wengi walivyokuwa wakitoa fedha na kuzitia katika hazina
ya Hekalu. Matajiri wengi walitoa fedha nyingi.
42 Hapo akaja mama mmoja mjane maskini, akatoa sarafu mbili
ndogo za fedha.
43 Yesu akawaita wanafunzi wake, akawaambia, "Kweli
nawaambieni, huyu mama mjane maskini ametoa zaidi kuliko wengine wote waliotia
fedha katika sanduku la hazina.
44 Maana wote walitoa kutokana na ziada ya mali zao, lakini
huyu mama, ingawa ni maskini, ametoa yote aliyokuwa nayo, ametoa kila kitu
alichohitaji kwa kuishi."
|