Chapter 3
1 Mwaka wa
kumi na tano wa utawala wa Kaisari Tiberio, Pontio Pilato alikuwa anatawala
mkoa wa Yudea. Herode alikuwa mkuu wa mkoa wa Galilaya, na Filipo, ndugu yake,
alikuwa mkuu wa mikoa ya Iturea na Trakoniti. Lusania alikuwa mkuu wa mkoa wa
Abilene,
2 na Anasi
na Kayafa walikuwa makuhani wakuu mjini Yerusalem. Wakati huo ndipo neno la
Mungu lilipomjia Yohane, mwana wa Zakariya, kule jangwani.
3 Basi,
Yohane akaenda katika sehemu zote zilizopakana na mto Yordani, akihubiri watu
watubu na kubatizwa ili Mungu awaondolee dhambi.
4 Ndivyo
ilivyoandikwa katika kitabu cha nabii Isaya: "Sauti ya mtu imesikika
jangwani: `Mtayarishieni Bwana njia yake; nyosheni mapito yake.
5 Kila
bonde litafukiwa, kila mlima na kilima vitasawazishwa; palipopindika
patanyooshwa, njia mbaya zitatengenezwa.
6 Na, watu
wote watauona wokovu utokao kwa Mungu."`
7 Basi,
Yohane akawa anawaambia watu wengi waliofika ili awabatize: "Enyi kizazi
cha nyoka! Ni nani aliyewadokezea kwamba mngeweza kuiepuka ghadhabu inayokuja?
8 Basi,
onyesheni kwa matendo kwamba mmetubu. Msianze sasa kusema: `Sisi ni watoto wa
Abrahamu.` Nawaambieni hakika, Mungu anaweza kuyageuza mawe haya yawe watoto wa
Abrahamu!
9 Lakini,
sasa hivi shoka limewekwa tayari kukata mizizi ya miti. Kila mti usiozaa
matunda mazuri utakatwa na kutupwa motoni."
10 Umati
wa watu ukamwuliza, "Tufanye nini basi?"
11
Akawajibu, "Aliye na nguo mbili amgawie yule asiye na nguo; aliye na
chakula afanye vivyo hivyo."
12 Nao
watoza ushuru wakaja pia ili wabatizwe, wakamwuliza, "Mwalimu, tufanye
nini?"
13 Naye
akawaambia, "Msitoze ushuru zaidi ya kima kilichowekwa."
14 Nao
askari wakamwuliza, "Na sisi tufanye nini?" Naye akawajibu,
"Msichukue vitu vya mtu yeyote kwa nguvu wala kumshtaki yeyote kwa uongo.
Toshekeni na mishahara yenu."
15 Wote
walikuwa wanatazamia kitu fulani; basi, wakaanza kujiuliza mioyoni mwao kuhusu
Yohane: kuwa labda yeye ndiye Kristo.
16 Hapo
Yohane akawaambia wote, "Mimi ninawabatiza kwa maji, lakini anakuja mwenye
uwezo zaidi kuliko mimi ambaye sistahili hata kumfungulia kamba za viatu vyake.
Yeye atawabatizeni kwa Roho Mtakatifu na kwa moto.
17 Yeye ni
kama mtu anayeshika mikononi mwake chombo cha kupuria nafaka, aipure nafaka
yake, akusanye ngano ghalani mwake, na makapi ayachome kwa moto
usiozimika."
18 Hivyo,
pamoja na mawaidha mengine mengi, Yohane aliwahimiza watu akiwahubiria Habari
Njema.
19 Lakini
Yohane alimgombeza Herode, mkuu wa mkoa, kwa sababu alikuwa amemchukua Herodia,
mke wa ndugu yake, na kumfanya mke wake; na pia kwa ajili ya mabaya yote
aliyokuwa amefanya.
20 Kisha
Herode akazidisha ubaya wake kwa kumtia Yohane gerezani.
21 Watu
wote walipokuwa wamekwisha batizwa, Yesu naye alibatizwa. Na alipokuwa akisali,
mbingu zilifunguka,
22 na Roho
Mtakatifu akamshukia akiwa na umbo kama la njiwa. Sauti ikasikika kutoka
mbinguni: "Wewe ndiwe Mwanangu mpendwa, nimependezwa nawe."
23 Yesu
alipoanza kazi yake hadharani, alikuwa na umri upatao miaka thelathini, na watu
walidhani yeye ni mwana wa Yosefu, mwana wa Heli.
24 Heli
alikuwa mwana wa Mathati, mwana wa Lawi, mwana wa Melki, mwana wa Yanai, mwana
wa Yosefu,
25 mwana
wa Matathia, mwana wa Amosi, mwana wa Nahumu, mwana wa Hesli, mwana wa Nagai,
26 mwana
wa Maathi, mwana wa Matathia, mwana wa Shemeni, mwana wa Yoseki, mwana wa Yuda,
27 mwana
wa Yohanani, mwana wa Resa, mwana wa Zerubabeli, mwana wa Shealtieli, mwana wa
Neri,
28 mwana
wa Melki, mwana wa Adi, mwana wa Kosamu, mwana wa Elmadamu, mwana wa Eri,
29 mwana
wa Yoshua, mwana wa Eliezeri, mwana wa Yorimu, mwana wa Mathati, mwana wa Lawi,
30 mwana
wa Simeoni, mwana wa Yuda, mwana wa Yosefu, mwana wa Yonamu, mwana wa Eliakimu,
31 mwana
wa Melea, mwana wa Mena, mwana wa Matatha, mwana wa Nathani, mwana wa Daudi,
32 mwana
wa Yese, mwana wa Obedi, mwana wa Boazi, mwana wa Salmoni, mwana wa Nashoni,
33 mwana
wa Aminadabu, mwana wa Admini, mwana wa Arni, mwana wa Hesroni, mwana wa
Feresi, mwana wa Yuda,
34 mwana
wa Yakobo, mwana wa Isaka, mwana wa Abrahamu, mwana wa Tera, mwana wa Nahori,
35 mwana
wa Serugi, mwana wa Reu, mwana wa Pelegi, mwana wa Eberi, mwana wa Sala,
36 mwana
wa Kainani, mwana wa Arfaksadi, mwana wa Shemu, mwana wa Noa, mwana wa Lameki,
37 mwana
wa Mathusala, mwana wa Henoki, mwana wa Yaredi, mwana wa Mahalaleli, mwana wa
Kenani,
38 mwana
wa Enosi, mwana wa Sethi, mwana wa Adamu, aliyekuwa wa Mungu.
|